Parliament of Tanzania

NAIBU SPIKA AKUTANA NA BALOZI WA CUBA.

Naibu Spika wa Bunge Mheshimiwa Dkt Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba hapa nchini Mheshimiwa Jorge Lopez Tormo leo tarehe 16 Disemba, 2015 jijini Dar es Salaam, ambapo Balozi huyo alimpongeza Mhe Dr Tulia kwa kuchaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Kumi na Moja.

Mbali na kumpa pongezi hizo Balozi Tormo pia alimuomba Naibu Spika kuanzisha ushrikiano baina ya Bunge la Cuba na la Tanzania kupitia ziara mbalimbali ambazo zitatoa fursa ya kubadilishana uzoefu pamoja na taarifa.

“Ni takribani miaka hamsini na tatu sasa toka Cuba na Tanzania zianzishe ushrikiano lakini katika kipindi chote hicho hapajawahi kufanyika ziara yoyote ya kibunge baina ya hizi nchi mbili, hivyo nadhani ni wakati mwafaka wa kufanya hivyo,” alisema Balozi Tormo.

Balozi Tormo ameahidi pia kuwa Serikali ya nchi yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika utoaji huduma bora za afya kwa kuwaleta madaktari bigwa nchini kuja kutoa huduma za afya ambapo inatarajia kuwaleta madaktari zaidi ya kumi mwakani pamoja na kusaidia katika ujenzi wa vituo vya afya.

Balozi Tormo alimueleza Naibu Spika kuwa Tanzania na Cuba imekuwa na uhusiano mzuri toka nchi ipate uhuru na kwamba kwa mawaka 2014 serikali yake ilileta madaktari zaidi ya 30 kuja kutoa huduma za afya katika maeneo mablimbali hapa nchini.

Aliongeza kuwa katika kuendeleza uhusiano huo Serikali yake itaendelea kuleta madaktari nchini kila mwaka kuja kutoa huduma za afya na kwa mwaka kesho wanatarajia kuleta zaidi ya madakatari kumi.

Balozi Tormo alimueleza pia Naibu Spika kuwa serikali yake ipo tayari kuendelea kuisaidia Tanzania hasa katika masuala ya afya ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya ili kuweza kuwasaidia watanzania walio wengi kupata matibabu yaliyo bora na ya gharama nafuu.

Kwa upande wake Naibu Spika Dkt Tulia alimshukuru Balozi Tormo kwa kwenda kumtembelea na kusema kuwa amefanya hivyo katika wakati muafaka ambapo Bunge jipya la Kumi na Moja ndo limenza na lipo katika harakati za kupanua wigo wa kushrikiana na Mabunge ya nchi nyingine.

Dkt Tulia pia alikubali ombi la Balozi Tormo la kuwapo kwa ushirikiano katika Bunge la Cuba na la Tanzania na kwamba watafanya hivyo kwa anzisha Chama Cha kirafiki wa Bunge la Cuba na la Tanzania.

“Ninafahamu kuwa uhusinao na ushirikiano baina ya Tanzania na Cuba upo vizuri lakini bado kuna mengi ambayo yannaweza kufanyiwa kazi ili tuwe zaidi ya tulivyo sasa,” alisema Dkt Tulia huku akisisitiza kuwa Bunge la Tanzania lipo tayari kuanzisha urafiki na Bunge la Cuba.

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's