Parliament of Tanzania

Mkutano wa Nane wa Bunge waanza Jijini Dodoma

Mkutano wa Nane wa Bunge la Kumi na Mbili la Jamhuri ya Muuugano wa Tanzania umeanza Jijini Dodoma ambapo katika Kikao cha Kwanza shughuli ya kwanza ilikuwa ni kuapa kwa Mbunge Mpya wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa (CCM) Mheshimiwa Tamima Haji Abass ambaye amechukua nafasi iliyoachwa na Marehemu Irene Alex Ndyamkama aliyeaga Dunia mwezi Aprili 2022.

Aidha katika Kikao cha Kwanza Spika wa Bunge Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) alitoa taarifa kwamba Miswada miwili ya Sheria iliyopitishwa wakati wa Mkutano wa Saba wa Bunge ambayo ni Muswada wa Matumizi ya Fedha wa Fedha za Serikali 2022 (The Appropriation Bill 2022) na Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2022 (The Finance Bill 2022) imeshapata kibali cha Mheshimiwa Rais na kuwa Sheria za nchi .

Aliongeza kuwa sheria hizo sasa zitaitwa; Sheria ya Matumizi ya Fedha (Na. 4) ya mwaka 2022 (The Appropriation (No. 4) Act 2022) na Sheria ya Fedha (Na. 5) ya mwaka 2022 (The Finance (No.5) Act 2022).

Mara baada ya taarifa hiyo Bunge liliendelea na kipindi cha Maswali na Majibu kabla ya kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa wa Mwaka 2022 (The Disaster Management Bill, 2022).

Kwa upande mwigine katika Mkutano huu, Bunge pia linatarajia kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.2) wa Mwaka 2022 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.2) Bill, 2022] pamoja na Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji wa Mwaka 2022 [The Water Resources Management (Amendment) Bill, 2022].

Mbali na hayo katika Mkutano huu, Bunge linatarajia kupokea na kuridhia; Azimio la Bunge Kuridhia Kufuta Hasara/Upotevu wa Fedha na Vifaa vya Serikali kwa kipindi kinachoishia tarehe 30 Juni, 2022, Azimio la Bunge Kuridhia Itifaki ya Mkataba wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Ugaidi ya Mwaka 2004 (Protocol to the OAU Convention on the Prevention and Combating of Terrorism, 2004) na Azimio la Bunge Kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuongeza Mamlaka ya Mahakama ya Afrika Mashariki

Shughuli nyingine zinazotarajiwa kufanyika wakati wa Mkutano huu ni Bunge kupokea taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo na Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA).

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

View All MP's