United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Mkutano wa Kumi wa Bunge umeanza Jijini Dodoma ambapo katika Kikao cha alimuapisha Mbunge Mteule wa Jimbo la Amani, Mheshimiwa Abdul Yussuf Maalim ambaye alichaguliwa baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo (Marehemu Mussa Hassan Mussa) kuaga dunia tarehe 13 Oktoba, 2022.
Kwa upande mwigine kabla ya
kuanza kwa Kipindi cha Maswali na Majibu katika Kikao cha Kwanza, Spika wa
Bunge alitoa taarifa juu ya Miswada mitatu ya Sheria ambayo imeshasainiwa na
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
Spika alisema Miswada hiyo ni
Muswada wa Sheria ya Uwekezaji ya Tanzania wa mwaka 2022, Muswada wa Sheria ya Ulinzi
wa Taarifa Binafsi wa mwaka 2022 na Muswada wa Sheria ya marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 3 wa
Mwaka 2022.
Alisema Miswada hiyo sasa
itatambulika kama Sheria ya Uwekezaji Tanzania namba 10 ya mwaka 2022, Sheria
ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi namba 11 ya mwaka 2022 na Sheria ya Marekebisho ya
Sheria Mbalimbali Na. 3 Sheria Namba 12 ya mwaka 2022.
Pamoja na mambo mengine, MKutano huu wa Kumi wa Bunge ni mahsusi kwa ajili ya Bunge kupokea na kujadili taarifa za mwaka za utendaji kazi wa Kamati za Kudumu za Bunge.