Parliament of Tanzania

Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yafunguliwa Jijini Arusha

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amefungua michezo ya Kumi na Moja ya Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inafanyika tarehe 4 hadi 17 Desemba, 2021 Jijini Arusha

Akifungua michezo hiyo Waziri Mkuu amesema Serikali za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zitaendelea kuchukua hatua za makusudi za kukuza michezo ndani ya jumuiya hiyo.

Amesema ni vyema Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zikaendelea kutumia majukwaa ya kimichezo kwa lengo la kubadilishana mawazo na kujadili kuhusu namna bora ya kuimarisha ushirikiano uliopo kwa ajili ya mustakabali na manufaa makubwa ya wananchi.

“Majukwaa ya namna hii yamekuwa chachu ya kuleta mwamko mkubwa wa masuala ya sanaa, burudani na michezo ndani ya jumuiya,” alisema.

Mheshimiwa Majaliwa aliongeza kuwa sekta ya michezo imekuwa chanzo kikubwa cha biashara, utalii, kuimarisha afya na ajira kwa vijana.

Aidha Waziri Mkuu aliwaasa Waheshimiwa Wabunge wabu kuendelee kuimarisha ushiriki wao kwenye masuala ya michezo kwani ina mchango mkubwa katika kuimarisha afya na hivyo kusaidia kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

“Nitoe rai kwa Bunge la Afrika Mashariki kusimamia kwa karibu ushiriki wa michezo kwa wabunge na hata wananchi wa Jumuiya yetu,” alisema.

Kaulimbiu ya Mashindano hayo ni “Strengthening Integration through Inter-Parliamentary Games in the Covid-19 era” yaani kuimarisha masuala ya mtangamano katika kipindi hiki cha UVIKO-19 kupitia Mashindano ya Mabunge ya Jumuiya.

Kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akizungumza kwa niaba ya Spika wa Bunge, alisema kuwa aliwaasa Wabunge washiriki katika mashindano hayo kuheshimiana katika michezo yote ili kuondoa mikanganyiko wakati wa ushindani

“Sote tuheshimiane anaposhinda mwenzako usione kwamba wewe ndio ulistahili kushinda, kwa hiyo tukashindane kama marafiki na ndugu na tuheshimiane ili pasitokee masuala ya kutoelewana,” alisisitiza.

Naibu Spika aliongeza kuwa Michezo hiyo ni kwa ajili ya kufahamiana na kuongeza uelewa kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa umuhimu wa kuwa wamoja.

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Mhe. Abbas Tarimba amesema Timu ya Bunge la Tanzania wameenda kushiriki na kushinda katika mashindano hayo hivyo shaba yao ni kuchukua Kombe katika kila mchezo watakaoshiriki.

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

Hon Salim Mussa Omar

Gando (CCM)

Contributions (1)

Profile

Hon. Rose Vicent Busiga

Special Seats (CCM)

Contributions (1)

Profile

Hon. Exaud Silaoneka Kigahe

Mufindi Kaskazini (CCM)

Questions / Answers(0 / 8)

Supplementary Questions / Answers (0 / 13)

Profile

View All MP's