Parliament of Tanzania

MHE MAKINDA ATANGAZA KUSTAAFU SIASA

Baada ya kulitumikia Taifa katika nafasi mbalimbali za uongozi kwa takribani miaka arobaini hatimaye aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Anne Semamba Makinda ametangaza rasmi kuwa hatagombea tena nafasi ya Uspika wa Bunge la Kumi na Moja.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam tarehe 13 Novemba 2015, Mhe Makinda amesema kuwa baada ya kulitumikia Bunge katika nafasi mbalimbali za uongozi katika vipindi tofauti akianza kama Waziri wa Shughuli za Bunge, Mwenyekiti wa Bunge, Naibu Spika na hatimaye Spika wa Bunge ameona ni vyema akang’atuka.
“Sitagombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, wala sitochukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika na wala sifikiri kwenda kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika,” alisema Mhe. Makinda.
Aidha aliongeza kuwa katika awamu yake akiwa kama Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kulikuwa na changamoto nyingi kutokana kuwapo kwa idadi kubwa ya Wabunge vijana.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

View All MP's