Parliament of Tanzania

MHE JOB NDUGAI ACHAGULIWA KUWA SPIKA

WABUNGE wa mkutano wa kwanza wa kikao cha kwanza cha Bunge la 11 wamemchagua Job Ndugai (Mb) kuwa Spika wa Bunge la 11 la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Ndugai anakuwa Spika wa 7 wa Bunge la Tanzania tangu uhuru, ambaye alipata kura 254 dhidi ya kura 109 za mshindani wake wa karibu Goodluck Ole Medeye kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akitangaza matokeo hayo leo Jumanne Novemba 17, 2015)

Mhe. Ndungai ambaye ni mbunge kutoka Jimbo la Kongwa, pia alikuwa Naibu Spika wa Bunge la Kumi la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania lililokuwa likiongozwa na Anne Makinda.

Mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, Ndugai alisema ataliongoza Bunge hilo kwa haki na usawa na hivyo kutoa nafasi kwa Wabunge kutoka vyama vyote vya siasa kushiriki katika mijadala mbalimbali ndani ya Bunge.

Aidha Ndugai alisema anafahamu umaskini, mahitaji na matarajio ya Watanzania, kuhusu nafasi ya chombo hicho katika kuisimamia Serikali, ambayo ni mojawapo ya jukumu la Bunge.

“Namuahidi Mhe. Rais kuwa Bunge hili litakuwa na ushirikiano na Serikali ya Awamu ya Tano kwa kusimamia kwa karibu shughuli zote za Serikali ili kunua uchumi wa nchi”

Kwa mujibu wa Ndugai alisema amepata uzoefu wa nafasi hiyo kutoka kwa Maspika watatu tofauti, ambao ni Pius Msekwa, Samwel Sitta na Anne Makinda, pamoja na kuongoza kamati mbalimbali za Bunge, hivyo kupitia uzoefu alioupata ataweza kufanya kazi hiyo kwa ufansi zaidi.

Akifafanua zaidi Ndugai alisema ataliongoa Bunge la 11 bila ubaguzi na demokrasia itachukua nafasi yake.

Kwa upande mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Goodluck Ole Medeye alisema hatma ya Watanzania ipo mikononi mwa Bunge hilo, hivyo wabunge hawana budi kutoa ushirikiano kwa Spika ili aweze kutimiza wajibu wake.

Wakiongea kwa wakati tofauti, wagombea wengine wa kinyang’anyiro cha nafasi hiyo, walitoa pongezi kwa Spika Ndugai na kumtaka kulifanya Bunge kuwa chombo chenye kuwaunganisha Wabunge wote na kuondoa misuguano na tofauti ya vyama ndani ya Bunge.

Jumla ya Wagombea 8 kutoka vyama vya AFP, CHADEMA, CCK, NRA, CCM, TLP, CHAUMMA, na DP waliwania nafasi hiyo, huku mgombea kutoka CHAUMMA, Hashim Rungwe akishindwa kutoka kufika katika uchaguzi huo pasipo na kutoa taarifa kwa msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Katibu wa Bunge.

Hata hivyo Wagombea kutoka katika vyama sita ambavyo ni AFP, CCK,NRA, TLP, CHAUMMA na DP hawakuweza kupata kura yoyote kati ya kura halali 363.

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

View All MP's