Parliament of Tanzania

KATIBU WA BUNGE AMEFUNGUA MAFUNZO YA WAKURUGENZI NA WAKURUGENZI WASAIDIZI

Katibu wa Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi, ndc amewataka wakurugenzi na wakurugenzi wasaidizi kufanya kazi kwa ushirikiano na watu walio chini yao na hivyo kulifanya Bunge kuwa sehemu nzuri ya kufanya kazi kwa wale wanaowatumikia.

Katibu wa Bunge alitoa rai hiyo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wakurugenzi na wakurugenzi wasaidizi wa Ofisi ya Bunge yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi, katika Ofisi Ndogo ya Bunge Zanzibar

“Sisi viongozi tunatakiwa kufanya Bunge kuwa sehemu nzuri ya kufanyia kazi na tunaowatumikia wawe na furaha,” alisema.

Aidha, alimshukuru Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai kwa kuona umuhimu wa mafunzo hayo hivyo kuwaruhusu viongozi hao wote kushiriki mafunzo.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Kadari Singo alimpongeza Bi. Nenelwa Mwihambi kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuteuliwa kushika nafasi ya Katibu wa Bunge.

Alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa viongozi hao kwa kuwa kwa taasisi waliyopo wanaushawishi katika namna moja au nyingine katika maendeleo ya Taifa.

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

Hon. Francis Kumba Ndulane

Kilwa Kaskazini (CCM)

Contributions (1)

Profile

Hon. Dr. Festo John Dugange

Wanging'ombe (CCM)

Questions / Answers(0 / 36)

Supplementary Questions / Answers (0 / 68)

Profile

Hon. Dr. Eliezer Mbuki Feleshi

None (Ex-Officio)

Profile

View All MP's