Parliament of Tanzania

Kamati za Kudumu za Bunge zaanza kukutana Jijini Dodoma

Kamati za Kudumu za Bunge zimeanza kukutana Jijini Dodoma kabla ya Mkutano wa Nane wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 13 Septemba, 2022.

Shughuli zilizopangwa kufanywa na Kamati katika vikao hivyo ni kama ifuatavyo:-

a. Kamati ya Sheria Ndogo itafanya Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa wakati wa Mkutano wa Saba wa Bunge.

b. Kamati Tisa (9) za Kisekta zitapokea na kujadili taarifa mbalimbali za utendaji.

c. Kamati mbili (2) zinazosimamia matumizi ya fedha za umma zitachambua Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2021.

d. Kamati tatu zitafuatilia utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yaliyotokana na Taarifa za Mwaka za Kamati zilizowasilishwa Bungeni Mwezi Februari, 2022.

e. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imepanga kupokea na kuchambua taarifa za uwekezaji wa mitaji ya umma ili kubaini iwapo uwekezaji huo una ufanisi na kuwa umezingatia taratibu na miongozo mujarabu ya biashara.

f. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama itapokea na kujadili Taarifa za Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki na za Wawakilishi wa Bunge la Tanzania katika Vyama vinne (4) vya Kibunge.

g. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imepanga kupokea na kujadili Taarifa ya yatokanayo na Kikao kilichofanyika kwa mujibu wa Kanuni ya 124(1) ya Kanuni za Bunge kwa ajili ya majumuisho ya hoja zilizojitokeza wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara kwa mwaka wa fedha 2021/2022 na Makadirio ya Matumizi ya Wizara hizo kwa mwaka wa fedha 2022/2023. Vilevile itapokea taarifa zinazoiwezesha Kamati kufuatilia ukusanyaji na vyanzo vya mapato nchini.

h. Kamati mbili (2) zitajadili miswada mitatu (3) ya sheria ikiwemo kupokea maoni ya wadau kuhusu miswada hiyo.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's