Parliament of Tanzania

Kamati yasikitishwa mradi wa ujenzi wa Nyumba za Watumishi kutelekezwa

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesikitishwa na kitendo cha kutelekezwa kwa miradi ya Nyumba nane za watumishi wa Wilaya za Mvomero na Wilaya ya Gairo.

Kamati hiyo ilisikitishwa na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miradi hiyo jana wakati ilipotembelea kujionea ujenzi wa Nyumba hizo ikiwemo nyumba za wakuu wa Wilaya hizo.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti aliyeongoza ujumbe wa Kamati hiyo, Shally Raymond alisema hawajaridhishwa na hatua ambayo ujenzi wa Nyumba hiyo ulipofikia.

"Kwa sasa nyumba hizi ni kama vile zimetelekezwa licha ya fedha nyingi za Serikali kutumika katika miradi hii," alisema.

Aidha, Kamati ilimuagiza Kaimu Meneja wa Mkoa wa Wakala wa Majengo (TBA), Edward Ngowi kuhakikisha inaipatia Kamati hiyo mapema iwezekanavyo mchanganuo wa fedha zilizotumika hadi sasa kwa kila nyumba badala ya kuleta gharama za jumla.

Alisema Kamati inataka mchanganuo huo ili kujua thamani ya fedha iliyotumika na kulinganisha na uhalisia wa miradi katika hatua iliyofikiwa.

Awali akitoa maelezo kuhusiana na miradi huo, Ngowi alisema hadi sasa mradi huo umeshatumia Sh. Milioni 184.4 .

Alizitaja changamoto zilizosababisha kukwama kwa utekelezaji wa miradi hiyo kwamba ni pamoja na ukosefu wa fedha kutoka Serikalini na kwamba zana ya ujenzi kwa gharama nafuu kuharibika kutokana na kutopatikana kwa fedha kwa wakati.


"Mradi umekosa fedha kwa muda mrefu na kuendelea kusababisha uharibifu kwa hatua iliyofikiwa na pia kuendelea kuongezeka kwa gharama za ujenzi," alisema.

Kwa mujibu wa Ngowi ujenzi huo ulianza katika Mwaka wa Fedha 2013/14 na ulitakiwa ukamilike ndani ya wiki 32 na kwamba hatua iliyofikiwa hadi sasa ni asilimia 30 huku fedha iliyotolewa ni asilimia 15

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

Hon. Mustafa Mwinyikondo Rajab

Dimani (CCM)

Profile

Hon. Abdullah Ali Mwinyi

Mahonda (CCM)

Contributions (2)

Profile

View All MP's