United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa A. Zungu awataka nchi za Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika kutoa vipaumbele kwa watu wenye ulemavu katika ngazi ya maamuzi.
Kauli hiyo ilitolewa Novemba 15, Jijini Dar-es-salaam akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa siku tatu wa Mtandao wa Wabunge Wenye Mahitaji Maalum wa Umoja wa Mabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA) Kanda ya Afrika (CPwD)
"Watu wenye ulemavu wanatakiwa kupewa vipumbele katika nyanja mbalimbali za kijamii ikiwemo katika vyombo vya maamuzi"
Naibu Spika alisema kwamba Mkutano huu utakuja na Maazimio ambayo yatakuwa na lengo la kuwezesha kimaendeleo wabunge wenye ulemavu na walemsvu wote kwa ujumla.
Alibainisha kuwa Tanzania imefika mahali pazuri kuwajali wenye ulemavu maana hata ujenzi wa miundombinu unazingatia hilo.
kwa upande wake Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu) Prof, Joyce Ndalichako alisema kwamba lengo la Mkutano huu ni kujadili namna watu wenye ulemavu hawaachi nyuma katika kujadili maendeleo.