United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
BUNGE limetangaza majina ya wabunge ambao wataliwakilisha katika Taasisi mbalimbali.
Wabunge waliochaguliwa ni pamoja na wajumbe watano wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambao ni Mh. Dk Pudensiana Kikwembe, Mh.Juma Othman, Mh. Mohamed Mchengelwa,Mh. Peter Serukamba na Mh. Susan Lyimo.
Wengine ni Wajumbe saba wa Tume ya Utumishi wa Bunge ambao ni Mh. Kangi Lugola, Mh. Mary Chatanda, Mh. Mussa Zungu, Mh.Hassan Turki
Mh. Magladela Sakaya na Mh.Peter Msigwa.
Kwa upande wa wawakilishi watano Katika Bunge la Afrika (PAP) waliochaguliwa ni Mh. Mboni Mhita, Mh. Dk. Faustine Ndugulile, Mh.Steven Masele, Mh. David Silinde na Asha Abdallah Juma ambaye anatoka Tanzania Viswani
Wajumbe watano wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-PF) Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai ataingia kwa nafasi yake huku wawakilishi wengine waliochaguliwa ni Mwenyekiti wa Wabunge Wanawake, Mh. Margareth Sitta, Mh. Jamal Kassim Ally, Mh. Esther Mnesi, Mh.Seleman Zedi na Mh. Ally Saleh.
Kamati ya utendaji ya Jumuiya ya Madola waliochaguliwa ni Mh. Amina Mollel, Mh. Maria Kangoye, Mh. Zainabu Vullu, Mh. Hamisi Ally na Mh. Salum Rehani.
Wengine ni Mh. Japhet Ngasonga, Mh. Jitu Son, Mh. Josephat Kandege na Mh. Dk Raphael Chegeni,Mh. Magreth Semesi, Mh. Juma Hamad Omar na Mh. Tundu Lissu.