Parliament of Tanzania

BUNGE LA VIJANA 2015 LAKUTANA DODOMA

Mkutano wa Pili wa Bunge la Vijana umefanyika mjini Dodoma kuanzia tarehe 15 – 19 Agosti 2015 kwa ushirikiano mkubwa kati ya Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Bunge hilo lililowakutanisha wanafunzi 110 kutoka vyuo vya elimu ya juu 21 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar lilijadili pamoja na mambo mengine upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na upatikanaji wa ajira kwa vijana baada ya kumaliza masomo.

Aidha, kulikuwepo na mjadala mpana wa hoja binafsi ya Mbunge kuhusu sera mpya ya elimu nchini hususan kipengele cha matumizi ya lugha ya Kiswahili kubaki kama lugha ya kufundishia na lugha ya Kiingereza kubaki kuwa somo tu la kawaida. Hoja hiyo iliamuliwa na wengi kuwa lugha ya Kiingereza itumike kufundishia.

Bunge la Vijana ambalo ni mwendelezo wa azimio la Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola (SADC-PF) linalenga kuwajengea vijana uwezo wa kujenga hoja, kuilinda na kuitetea. Aidha, ni jukwaa maridhawa linalowakutanisha vijana wasomi ili kujadili mustakabali wa taifa lao huku wakijikita katika hoja zenye kuliletea taifa tija.

Kwa upande wa Ofisi ya Bunge, Bunge la Vijana ni kitalu maridhawa cha kuwaandaa viongozi kwani katika kuhoji, kujadili kwa nidhamu, kushirikishana, kufuata taratibu.


Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

View All MP's