Parliament of Tanzania

Bunge la Tanzania na India kuendeleza ushirikiano

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Wananchi wa India Shri Om Birla, huku jambo kubwa likiwa kuendeleza ushirikiano kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya afya.

Akizungumza mbele ya Spika huyo wa Bunge la Wananchi wa India leo Januari 18,2023 katika Ofisi ndogo za Bunge zilizopo Jijini Dar es Salaam , Dkt.Tulia amesema kwamba ugeni wa Spika huyo ni wa kihistoria kwani imepita miaka 50 tangu ujio wa aina hiyo mwaka 1961.


Dkt. Tulia amesema wamezungumza mambo mengi ikiwemo ushirikiano wa kibunge kati ya Bunge la Tanzania na Baraza la Wawakilishi upande wa Zanzibari pamoja na Bunge la Wananchi wa India.


"Kwa hiyo tumezungumzia kuhusu ushirikiano katika mambo mengi na kwa upande wa Bunge tumezungumza kuamsha uhusiano uliokuwepo kati ya Mihimili hii lakini kuweza kutumia chuo cha mafunzo ambacho wao wanacho, Mafunzo ambayo yanatolewa na Chuo hicho ni kwa ajili Wabunge pamoja na wafanyakazi wa Bunge la Wananchi wa India." Amesema Dkt. Tulia


"Mambo mengine ambayo tumeyazungumza ni utayari wa Bunge la India kushirikiana na Baraza la Wawakilishi Kwa maana ya Zanzibar pamoja na kushirikiana na Bunge la Tanzania kwenye eneo hilo, Kuhusu nchi zao mbili katika ushirikiano uliopo tangu miaka ya 1960 ambapo India na kama mnavyofahamu inajulikana kama mama wa demokrasia" amesisiza Dkt. Tulia.


Kwa upande wake wa Spika wa Bunge la Wananchi wa India Shri Om Birla ametumia nafasi hiyo kueleza masuala mbalimbali ambayo wameyazungumza na miongoni mwa sekta ambazo wamezungumza ni sekta ya kilimo, maji, afya na teknolojia huku akisisitiza kuhusu matumizi ya Teknolojia katika kilimo.


Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's