Parliament of Tanzania

UTEUZI WA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kesho tarehe kesho Alhamisi tarehe 21 Januari, 2016 atafanya uteuzi wa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge na kufuatiwa na Uchaguzi wa Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati husika pamoja na Kamati kupatiwa maelezo juu ya Wajibu, kazi na Mipaka ya kazi ya Kamati na kupokea na kujadili Mpango kazi wa Kamati unaoishia Juni, 2016.

Kwa kuzingatia Kanuni ya 111 ya Kanuni za kudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013 siku ya Ijumaa tarehe 22 hadi Jumamosi tarehe 23 Januari kutakuwa na Mkutano wa Wabunge wote ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na lengo la kuwafahamisha Wabunge kuhusu Kanuni za Kudumu za Bunge na Uendeshaji wa Bunge, Nadharia ya mgawanyo wa Madaraka katika Mihimili ya Dola, Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na Mambo Mengine ya Kiserikali.

Aidha, Kikao cha kwanza cha Kamati ya Uongozi ambacho wajumbe wake ni Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge chini ya Uenyekiti wa Mhe. Spika, kinatarajiwa kufanyika Siku ya Jumapili tarehe 24 Januari, 2016, ambapo Jumatatu tarehe 25 Januari, 2016 itakuwa ni siku mahususi kwa Wabunge kupata maelezo kuhusu Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano. Ratiba ya Shughuli za Mkutano wa pili wa Bunge unaotarajiwa kuanza Jumanne tarehe 26 Januari, 2016 itatolewa baadae.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

Hon. Juliana Didas Masaburi

Special Seats (CCM)

Contributions (1)

Profile

Hon. Suma Ikenda Fyandomo

Special Seats (CCM)

Contributions (2)

Profile

View All MP's