Parliament of Tanzania

UPINZANI WATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI KIVULI

KIONGOZI wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe leo ametangaza Baraza Kivuli la Mawaziri ambalo lina jumla Wizara 19.

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Waziri ni Mh. Jaffary Michael na Naibu wake Mh. Joseph Makundi.

Ofisi ya Rais Utumishi Waziri ni Mh.Ruth Mollel,Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Waziri ni Mh. Ally Salehe Abdallah Ally na Naibu Wake ni Mh.Pauline Gekul.

Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi na Ajira Waziri ni Mh. Esther Bulaya Manaibu wake ni Mh. Yusuf Kaiza Makame na Mh. Maftaha Abdalla Nachuma.

Wizara ya Fedha na Mipango Waziri Waziri ni Mh. Halima Mdee , Naibu Waziri ni Mh.David Silinde. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Waziri ni Mh. Jmaes Francis Mbatia Naibu wake ni Mh.Willy Quambalo.

Wizara ya Madini Waziri ni Mh. John Mnyika na Naibu wake ni Mh.John Heche, Wizara ya Mambo ya Nje,Afrika Mashariki na Mahusiano ya Kimataifa Waziri ni Mh.Peter Msigwa na Naibu wake ni Mh.Riziki Shahali Mngwali na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Waziri wake ni Mh. Juma Hamad Omar na Naibu ni Mh. Mwita Mwikabe Wiatara.

Nyingine ni Wizara ya Mambo ya Ndani Waziri ni Mh. Godbless Lema na Naibu ni Mh. Masoud Abdallah Salim, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Waziri ni Mh. Wilfrey Lwakatare na Naibu wake ni Mh. Salma Mohamed Mwasa.

Wizara ya Maliasili na Utalii itaongozwa na Mh. Esther Matiko na Naibu wake ni Mh.Cecilia Presso, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Waziri ni Mh. Anthony Komu na Naibu wake ni Mh. Cecil Mwambe, Wizara ya Elimu, Teknolojia na Ufundi Waziri ni Mh. Susan Lymo na Naibu Waziri ni Mh. Dk. Ally Suleiman Yusuf.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Waziri ni Mh. Dk. Godwin Mollel na Naibu wake ni Mh. Zubeda Sakuru, Wizara ya Habari, Utamaduni naMachezo Waziri ni Mh. Joseph Mbilinyi na Naibu wake ni Mh. Devotha Minja.

Wizara ya Maji na Uwagiliaji Waziri ni Mh. Hamidu Hassan Bobali na Naibu wake ni Mh.Petea Lijua-likali na Wizara ya Katiba na Sheria Waziri ni Mh. Tundu Lissu

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

Hon. Kassim Majaliwa Majaliwa

Ruangwa (CCM)

Questions / Answers(0 / 1)

Contributions (7)

Profile

Hon. Dr. Alfred James Kimea

Korogwe Mjini (CCM)

Supplementary Questions / Answers (1 / 0)

Contributions (1)

Profile

Hon. Ravia Idarus Faina

Makunduchi (CCM)

Profile

Hon. Amina Daud Hassan

Special Seats (CCM)

Profile

View All MP's