Parliament of Tanzania

Serikali yawasilisha Mapendekezo ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti kwa Mwaka 2016/17

Serikali imewasilisha mapendekezo ya kiwango na ukomo wa Bajeti yake kwa mwaka 2016/17 kwenye mkutano wa Wabunge wote katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kabla ya Waziri wa Fedha na Mipango kuwasilisha mapendekezo hayo Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai alisema lengo kubwa la mkutano huo ni kutekeleza matakwa ya Kanuni ya 97 (1) na (2) ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari, 2016 inayoelekeza kuwa tarehe kumi na moja ya kila mwaka, au siku nyingine ya kazi inayofuata iwapo tarehe hiyo itakuwa siyo ya kazi, Waziri anayehusika na masuala ya Mipango atawasilisha kwa Wabunge Mapendekezo ya Serikali ya Mapngo kwa mwaka wa Fedha unaofuata.

Aidha, katika tarehe hiyo Waziri anayehusika na masuala ya fedha atawasilisha kwa Waheshimiwa Wabunge Mapendekezo ya Serikali ya kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha unaofuata.

Mhe. Spika wa Bunge alisema pia kuwa tarehe 11 Machi, 2016 Waheshimiwa Wabunge walio wengi walikuwa Majimboni wakitekeleza majukumu yao baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Pili Bunge hivyo Mkutano wa Wabunge wote kwa ajili ya Mapendekezo ya Mpango kuwasilishwa usingeweza kufanyika.

Mhe Ndugai aliongeza kwa kwa kutumia mamlaka aliyopewa na Kanuni ya 5 (1) ya kanuni za Bunge na baada ya kufanya mashauriano na Serikali alielekeza Mkutano huo ufanyike tarehe 6 Aprili, 2016.

“Kwa mujibu wa Kanuni ya 97 (3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge shughuli yaio leo ni kupokea tu Mapendekezo hayo na kakutakuwa na majdala wowote. Hivyo basi, mara baada ya kupokea mapendekezo hayo Waheshimiwa Wabunge wataombwa kurejea kwenye majukumu yao mengine kwa kwa mujibu wa ratiba za Kamati zao,” alisema Spika wa Bunge.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's