Parliament of Tanzania

Ofisi ya Bunge yawasilisha Mapendekezo ya Bajeti mbele ya Kamati ya Bajeti

Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah amewasilisha Mapendekezo ya makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa Fedha 2016/17 mbele ya Kamati ya Bunge ya Bajeti ikiwa ni matakwa ya kisheria kwa Mfuko wa Bunge kuandaa Bajeti kabla ya kuwasilishwa na kupitishwa Bungeni.

Katika utaratibu wa maandalizi ya Bajeti ya Bunge sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 imeweka masharti chini ya kifungo cha 71 kwa Bunge kuwasilisha makadirio hayo katika kikao cha Mashauriano baina ya Kamati ya Bajeti na Waziri wa Fedha

Kulingana na ratiba ya shughuli za Kamati za Bunge, Serikali itawasilisha dondoo na randama za vitabu vya bajeti kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na kufuatiwa na mkutano wa Wabunge wote kupokea mapendekezo ya Mpango na kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na kufuatiwa na kamati ya Bajeti kuanza uchambuzi wake katika mapendekezo hayo kabla ya kuanza vikao vya mashauriano na serikali kuhusu Bajeti ya mwaka ujao.

Aidha, kwa mujibu wa sheria hiyo ya Bajeti, Mifuko mingine iliyowasilisha Bajeti zao mbele ya Kamati ya Bunge ya Bajeti ni pamoja na Mfuko wa Mahakama ambao unapendekeza Bajeti ya Mahakama kwa mwaka 2016/2017 na Ofisi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.


Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's