Parliament of Tanzania

Mkutano wa Tano wa Bunge waanza Jijini Dodoma

Mkutano wa Tano wa Bunge la Kumi na Mbili mahsusi kwa ajili ya kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 umeanza Jijini Dodoma.

Akizungumza Bungeni katika Kikao cha Kwanza, Spika wa Bunge, Mhe. Job Y. Ndugai (Mb) alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameshasaini Miswada Mitano (5) iliyopitishwa na Bunge katika Mkutano wa Nne kuwa Sheria.

Alizitaja Sheria hizo kuwa ni pamoja na Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Usajili wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu wa mwaka 2021, Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2021 na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 4) wa Mwaka 2021.

Sheria nyingine ni ya Marekebisho ya Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Mwaka 2021 na Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 5) wa Mwaka 2021.

Katika kikao kicho cha Kwanza cha Mkutano wa Tano, Mhe. Spika aliwaapishwa Wabunge watatu wapya ambao ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emanuel Cherehani na Mbunge wa Jimbo la Konde, Mhe. Mohammed Said Issa.

Aidha katika siku ya kwanza ya Bunge Waheshimiwa Wabunge walipata fursa ya kupokea maelezo kuhusu Maeneo ya Vipaumbele ya Matumizi ya Fedha za Mkopo nafuu wa IMF kwa ajili ya kukabiliana na athari za UVIKO-19 kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba katika Ukumbi wa Msekwa.

Kwa mujibu wa ratiba katika kipindi hiki cha Bunge, Waheshimiwa Wabunge wanatarajiwa kupewa mafunzo kuhusu fursa ya Uwekezaji katika Mifuko ya pamoja, Soko la mitaji na uzoefu wa Biashara na Ujasiriamali.

Mbali na hayo Waheshimiwa Wabunge pia wanatarajiwa kupokea maelezo kuhusu Miradi ya Nishati ya Umeme ya kimkakati na hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wake katika Ukumbi wa Msekwa.

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

View All MP's