Parliament of Tanzania

MHE. SPIKA APOKEA NA KUZIKABIDHI SERIKALINI TAARIFA ZA KAMATI MAALUM

Spika wa Bunge, Mhe. Job Y. Ndugai (Mb), amepokea na kukabidhi Serikalini Taarifa za Kamati Maalum alizounda kuchunguza na kushauri kuhusu sekta ya Uvuvi wa Bahari Kuu na Gesi Asilia.


Taarifa hizo zilipokelewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa kwa niaba ya Waziri Mkuu.

Halfa hiyo ya makabidhiano ilifanyika katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma Juni 2, mwaka 2018 na kuhudhuriwa na Waheshimiwa Wabunge na viongozi mbalimbali wa
Kitaifa.


Taarifa ya Kamati Maalum ya Sekta ya Uvuvi wa Bahari Kuu iliwasilisha
na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Anastazia Wambura na kwa upande wa Kamati
Maalum ya Nishati ya Gesi aliwasilisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.
Dunstan Kitandula.

Akizungumza mara baada ya kuwasilishwa kwa taaarifa za Kamati hizo,
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai alisema kuundwa kwa Kamati hizo ni
kutimiza wajibu wa Wabunge kuisimamia na kuishauri Serikali hasa
katika maeneno ambayo bado hayana mchango wa kutosha katika
kuinufaisha nchi.

“Nawashukuru wajumbe wa Kamati zote mbili kwa kazi nzuri iliyotukuka,
tatizo kubwa tumeona lipo katika mikataba, inatuumiza sana,” alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, Mhe.
Profesa Makame Mbarawa alimshukuru Mhe. Spika kwa uzalendo wake kwa
kuwa bila yeye ripoti hizo zisingekuwepo.

Aliwashukuru pia Wenyeviti wa Kamati zote mbili na wajumbe wake kwa
kufanya kazi kwa uzalendo usiku na mchana na kutoa ripoti zilizosheheni
mapendekezo ambayo yakifanyiwa kazi nchi itasonga mbele.

“Tutasoma kila kitu katika ripoti hizo na kuwahakikishia kwamba
mapendekezo yote yatatekelezwa kwa ukamilifu ndani ya muda mfupi,
wahusika wote waliotajwa kwa tuhuma mbalimbali kwenye ripoti, uchunguzi
utafanyika na sheria itachukua mkodo wake,” alisema.

Mhe. Spika aliunda kamati hizo Novemba 17 kwa lengo la kuchunguza na
kushauri sababu za sekta hiyo kutochangia ipasavyo katika Pato la
Taifa.


Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

View All MP's