Parliament of Tanzania

Kamati za Kudumu za Bunge zaanza kukutana Mjini Dodoma

Kamati za Kudumu za Bunge zimeanza kukutana Mjini Dodoma kutekeleza majukumu yake kuanzia Tarehe 20 Machi, 2017 hadi Tarehe 2 Aprili, 2017 kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Saba wa Bunge uliopangwa kuanza Tarehe 4 April 2017.


Katika kipindi hiki Kamati zitatembelea maeneo mbalimbali nchini kukagua miradi ya maendeleo iliyotengewa fedha kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 inayotekelezwa na Wizara/Idara zinazosimamiwa na Kamati husika.


Baada ya ziara hizo kukamilika,Kamati zitachambua Taarifa za utekelezaji wa Bajeti za Wizara inazozisimamia kwa Mwaka wa Fedha unaoisha kwa ajili ya kufanya ulinganisho kuhusu makadirio ya matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha unaofuata.


Aidha, kulingana na matakwa ya kikanuni, Tarehe 28 Machi, 2017 kutakuwa na Mkutano wa Wabunge wote kwa ajili ya kupokea Mapendekezo ya Serikali kuhusu Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's