|
|
| Home »Supplementary Question |
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Ruhwanya, Mhonga Said[CHADEMA]
Special Seat |
|
|
|
|
|
|
| 10 |
1 |
PRIME MINISTER'S OFFICE (POLICY, COORDINATION AND PARLIAMENTARY AFFAIRS) |
Central Government |
29 January 2008 |
Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza moja la nyongeza.
Kwa kuwa kote walikokwenda Mawaziri kuna Wabunge na Wabunge kazi yao ni kuwakilisha wananchi, kupeleka maelezo ya Serikali au majibu ya hoja zao, sasa Mawaziri wakifanya kazi hiyo Wabunge wafanye kazi gani?
|
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 1
SESSION # 10 |
 |
Answer From Hon.Burian, Dr. Batilda Salha
PRIME MINISTER'S OFFICE (POLICY, COORDINATION AND PARLIAMENTARY AFFAIRS) |
|
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU:
Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, ni vizuri tukatambua kwamba Wabunge wana wajibu mkubwa katika Majimbo yao lakini ni vizuri pia wananchi wakaelewa kwamba pamoja na wajibu mkubwa walionao Wabunge lakini wana rasilimali chache sana za kuwawezesha kutekeleza wajibu huo kwa ufanisi unaokusudiwa. Ndiyo maana katika Bunge hili tunajitahidi na tulitaka tuhakikishe kwamba tunaweza kuwapatia fursa ya kuweza kuwafanya mkazunguka. Sasa Mawaziri walivyokwenda kule ni wajibu wa Serikali kuhakikisha kwamba yale ambayo wanayapanga yanatekelezwa kwa ufanisi uliokusudiwa. Wabunge kazi yao kwenda kule ni kufuatilia kuhakikisha kwamba ule utendaji na ahadi zile kweli zinatekelezwa.
Kwa hivyo uhusiano wa Wabunge na Serikali ni uhusiano wa ushirikiano yaani ku-compliment initiative za Serikali. Kwa hivyo, hata siku moja hatutaweza kusema kwamba Serikali itakaa chini kutokufanya ziara eti kwa sababu kuna Wabunge katika Majimbo. Wabunge wataendelea kufanya kazi na Serikali itaendelea kuhakikisha kwamba inawapatia Wabunge rasilimali mbalimbali za kuhakikisha kwamba wanafanya kazi zao katika Majimbo yao lakini Serikali itafuata wananchi wale ambao waliwapa kura na kuhakikisha kwamba yale ambayo waliwaahidi wanatekeleza kadri ilivyokusudiwa. |
|
Records 1 to 1 of 41 |
|
|
|
|
|