|
|
| Home »Supplementary Question |
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Keenja, Charles N.[CCM]
Ubungo Constituency |
|
|
|
|
|
|
| 11 |
103 |
COMMUNICATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY |
Communication/Infrastructure |
17 April 2008 |
| Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niulize swali moja la nyongeza. Kutokana na kubadilika sana kwa teknolojia ya mawasiliano ambayo inafanya baadhi ya kazi zilizokuwa zinafanywa na Shirika la Posta zisiwe na maana sasa hivi, je, ni ubunifu gani unaofanywa na Wizara na Shirika hili kuhakikisha kwamba linajiendesha kibiashara na kwa faida? |
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 103
SESSION # 11 |
 |
Answer From Hon.Daftari, Dr. Maua Abeid
COMMUNICATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY |
|
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli teknolojia ya Posta sasa inahitaji mabadiliko makubwa sana kwa sababu teknolojia tuliyo nayo sasa hivi ya internet inachukua nafasi kubwa sana kwa kazi ambazo Posta inafanya. Tayari tumeshawapa changamoto wenzetu ya kuona wanaweza kufanya nini ili kuendana na wakati huu.
Zamani watu walikuwa wanatuma vifurushi na barua kwa kutumia Posta, sasa hata kadi za mwaliko zinatumwa kwa kutumia internet. Kwa maana hiyo, wanachofanya sasa watu wa Posta ni kuhakikisha kwamba wanakuwa na mitandao ya mawasiliano nchi nzima kwa kutumia computer, zile huduma ambazo zinaweza kutolewa za ICT kama huduma za Internet Caf sasa zipatikane katika sehemu zote za Posta, tunaanza na Mkoa, tutakuja Wilaya, halafu tutakuja na sehemu nyingine zilizobakia.
Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuongeza mapato wanataka kufanya utafiti wa soko ili kujua mahitaji, lazima kama mfanyabiashara ujue mteja wako anataka nini, mionjo gani iliyoko hivi sasa, huwezi kumwambia mtu sasa hivi anataka kunywa soda wakati kuna baridi, hatotaka soda na haitauzika.
Kwa hiyo, na wao wamo katika shughuli hizi za kujiendesha kibiashara, lakini pia kuwa mawakala wa taasisi na mashirika mbalimbali kwa mfano, kama kunatakiwa kulipiwa bill za umeme au za maji, wao wawe mawakala wa kuzipeleka, halafu wao wanapata chochote. Hizi ni mbinu za kibiashara ambazo ziko nyingi, lakini zinahitaji fedha na fedha hizo tutazipitisha katika Bunge hili. Kwa hiyo, nitawaomba Waheshimiwa Wabunge waniunge mkono katika hili ili Posta nayo sasa iweze kusimama kwa miguu yake.
|
|
Records 1 to 1 of 19 |
|
|
|
|
|