ASK THE SPEAKER
GIF

Hon.Samuel Sitta(MP)
Online interactive forum with the SPEAKER
QUOTES FROM THE SPEAKER
" One of the core duties of the Legislature is to oversee the functions of the Government in power and advise it appropriately whenever any pertinent issue of national interest arises. "
5th March 2009 - Dar es Salaam.
INVITATION FOR TENDERS
Tender for the Financial year 2010/2011
Read more
RESOURCES LINKS

Parliamentary Resources
National Website
Prime Minister's Office website
National Electoral Commission website
Africa4All project

WEBMAIL LOGIN


NEWSLETTER
Subscribe to our e-newsletter and be the first to know about new activities, events and resources.
Your email
GLOSSARY
Government policy
This is a plan of action that the government proposes to take, eg, to ban smoking in all public places.
Amendments
When Members of the Parliament are debating or examining Bills they often want to change some of the details. They can therefore propose changes or amendments, and debate and vote on them in the House. konya haber konhaber
Read more
VISITORS TO THIS SITE
There have been 30572118 visitors to this websiteThere have been 30572118 visitors to this websiteThere have been 30572118 visitors to this websiteThere have been 30572118 visitors to this websiteThere have been 30572118 visitors to this websiteThere have been 30572118 visitors to this websiteThere have been 30572118 visitors to this websiteThere have been 30572118 visitors to this website
User online : 12
Home »Pm questions & answers
Pm questions & answers
  email E-mail this to a friend email Printable version
Date Session Sitting
28 January 2010 18 3
Hon Mohamed, Hamad Rashid[CUF]
Mheshimiwa Spika, ahsante. Mheshimiwa Waziri Mkuu nafikiri unakumbuka tarehe 5 Novemba, 2009 Dr. Aman Abeid Karume na Maalim Seif Sharif Hamad, walikutana na hatimaye chama cha CUF kikamtambua na kuitambua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ni nini position ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya maridhiano haya?
Answer From Prime Minister
Mheshimiwa Spika, wako watu watatu au wanne wakisimama najua ni yaleyale tu.

Mheshimiwa Spika, sina hakika kama nitakuwa na jibu zuri sana, lakini niseme kwamba tunao mfumo mzuri sana wa namna ya kufanya maamuzi makubwa kama haya. Sasa ni kweli jambo hili limetokea pale Zanzibar lakini mimi imani yangu ni kwamba katika kutekeleza ule mfumo wa namna ya kufanya maamuzi yafikie ukomo wake naamini ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kwa kutumia Kamati maalumu ya Chama cha Mapinduzi ndani ya Zanzibar bila shaka jambo hili litakuwa tayari limeshazungumzwa, ndiyo imani yangu mimi.

Naamini vilevile kwamba baada ya hapo hatua itakayofuata ni kulileta jambo hili sasa formally kwenye Chama cha Mapinduzi kupitia Kamati Kuu pamoja na Halmashauri Kuu ya Taifa. Kwa hiyo, kama ni jibu sahihi juu ya nini mtazamo wa Serikali itakuwa ni baada ya chama kuwa kimefanya maamuzi na kuielekeza Serikali ifanye nini katika jambo hili.

Kwa hiyo, mimi naamini kabisa tutakapofika hatua hiyo ukiniuliza Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed mimi nitakuambia kimesemwa nini kama Serikali lakini ukiniuliza tu kwamba maoni yako wewe kama Pinda unasema nini na mimi ningesema vilevile kwamba kama Watanzania wengi wanavyofikiria kwamba ni jambo jema na mimi nafikiri ni jambo jema kwa maana tungependa Zanzibar ikawa na yenyewe ni eneo la utulivu na amani badala ya kukaa mnavutanavutana.
Hon Mohamed, Hamad Rashid[CUF]
Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati yuko Egypt baada ya kupata taarifa hizi alitoa salamu na kuunga mkono hatua hii na hatimaye katika hotuba zake mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya mwisho wa mwezi vilevile aliliunga mkono. Je, haionekani hiyo tayari ni position ya Serikali?
Answer From Prime Minister
Mheshimiwa Spika, nchi yoyote mnayokuwa na Rais mwenye madaraka wanamuita Executive President yeye kusema kweli ndiye anaweza kusema jambo lolote juu ya nchi yake. Kwa hiyo, yeye alikuwa analisema kama kiongozi wa nchi hii na mimi napenda niamini kwa dhati kwamba ni imani yake kwamba jambo hili lina ubora na ukiniuliza mimi nitasema pengine ni kiashiria kizuri kwamba hata likija kwenye chama na pengine kwenye Serikali tunadhani wote tutakwenda na msimamo wa namna hiyo. Mimi nadhani ndiyo fikra zangu zinakonituma.
Hon Nkumba, Said Juma[CCM]
Mheshimiwa Spika, naomba nimuulize swali Mheshimiwa Waziri Mkuu.
Kwa kuwa, baadhi ya migogoro ya mipaka hapa nchini inachukua muda mrefu sana kupatiwa ufumbuzi na kuwaacha wananchi wa maeneo haya wakishindwa kuaminiana na kuishi kwa uhasama na kwa kufanya hivi basi migogoro inasababisha kukwama kwa huduma za maendeleo, na kwa kuwa mgogoro wa mpaka wa Manyoni na Sikonge Mheshimiwa Waziri Mkuu unaufahamu vizuri tangu ukiwa Naibu Waziri halafu ukawa Waziri halafu leo Waziri Mkuu. Mgogoro huu umedumu takribani miaka 20, naomba nikuulize Serikali inasema nini juu ya kuamua sasa na kutoa maamuzi ambayo yatahitimisha mgogoro huu uliodumu kwa muda mrefu sana?
Answer From Prime Minister
Mheshimiwa Spika, mimi Bungeni humu nina miaka kidogo sana sijafika hata hiyo miaka 15, lakini anachosema ni kwamba inaonekana ni muda mrefu wamekuwa wakivutana, ni kweli kwamba nimekuja nikalikuta kama Naibu Waziri na nilikwenda pale tukafanya juhudi za awali na bado naamini litatafutiwa ufumbuzi.

Mheshimiwa Spika, lakini matatizo haya ya mipaka ndani ya nchi kati ya kijiji na kijiji, kata na kata au tarafa na tarafa au Wilaya na Wilaya, mkoa na mkoa katika mazingira ya kawaida halipaswi kuwa jambo kubwa kiasi cha kutufikisha mahali tukaanza kuhatarisha hata usalama wa wananchi, hata kidogo!

Tatizo ninaloliona tu ni kwamba mara nyingi Viongozi wa kisiasa ndiyo tunaolikuza sana hili jambo kwa sababu upande mmoja uking’ang’ania msimamo fulani hautaki kuona kwamba pengine kinachohitajika hapa ni suluhu tena ni suluhu ya haraka.

Sasa kwa swali la Mheshimiwa Nkumba ni kweli kwamba kuna mgogoro kati ya Manyoni na Sikonge katika Kijiji kimoja cha Kalangali, suala pale ni kama Kalangali iko Sikonge ama iko Manyoni. Kijiji cha Kalangali kinapata huduma zake zote Manyoni kwa sababu kiko karibu zaidi na Wilaya ya Manyoni, na kiko mbali na Makao Makuu ya Sikonge. Sasa kwa maana ya mpaka inaonekana Kalangali iko Sikonge lakini kwa maana ya hali ya uhalisia ulivyo kwa kweli Kalangali iko Manyoni kwa madhumuni yote, kinachohitajika hapa ni pande hizi mbili kukaa na kukubaliana kwamba hawa wana Kalangali acheni waendelee kuhudumiwa na Manyoni, acheni waendelee kupiga kura Manyoni kwa sababu mipaka haiwezi kuwa ndiyo ukuta kati ya Wilaya ya Sikonge na Wilaya ya Manyoni.
Sasa nimemwambia Mheshimiwa Nkumba na wenzake kwamba kaeni chini mkiridhiana hili mkaelewana hivyo halina tatizo kwanza sisi wengine wote tutanyamaza kwa sababu litakuwa limekwisha, lakini kama mtaamua kwamba Kalangali lazima iende Sikonge na wenyewe wanasema Sikonge hakuna huduma, tuko mbali mno sisi tutaendelea kuwa Manyoni hamtalimaliza hata kidogo.

Kwa hiyo, mimi naomba Mheshimiwa Nkumba kwamba kaeni pande zote mbili. Mimi ukiniuliza sasa ninaona suluhu nzuri kabisa ni kwenda kule ambako kimsingi huduma zinapatikana acheni wafuate huduma zao pale. Suala la mpaka ni kwenye makaratasi na kwa madhumuni ya utawala ikibidi tutamuomba Rais akiridhia kwamba tupindishe mpaka sasa tutafanya lakini kwa madhumuni ya zoezi hili mimi nadhani hiyo ndiyo ingekuwa njia sahihi na ya kweli.
  Records 1 to 3 of 7
 
Next Last
WHO IS WHO
Hon.Massaburi, Janeth Mourice
bunge
Questions(17)
Supplementary Questions(12)
Contributions(58)
More Members »


POLIS DATABASE
polis
BUDGET 2010/11
Estimate of Public Expenditure Development votes and supply vote
SEARCH FOR MP
Region
Constituent
 
VIDEO /AUDIO CLIP
More Videos
PHOTO GALLERY
Police parading(Saluting)the President Jakaya Kikwete when arrived to the Bunge Complex in Dodoma on 21.8.2008.
More photos
CALENDAR OF EVENTS
 <<  < Sep 2010 >   >>
SMTWThFS
1234
5678
9
1011
12131415161718
19202122232425
2627282930

More events

Copyright © 2003-2008 Tanzania Parliament. All rights reserved.
Designed and published by DataVision International (T) Ltd
Terms of Use | Disclaimer