|
|
| Home »Pm questions & answers |
|
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
|
 |
Hon Mohamed, Hamad Rashid[CUF] |
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, jana wakati Kamati ya Nishati na Madini ikiwasilisha hoja, moja katika hoja namba 18 ilielekeza kwamba Serikali ichukue hatua za kisheria za kuwashitaki watu wa Richmond, na Serikali katika maelezo yake ikasema kwamba uchunguzi wa ndani umemalizika lakini uchunguzi wa nje haujakamilika.
Katika suala la Rada, Serikali ilikuwa ikishirikiana na Serious Fraud Organisation ya Uingereza ili iweze kupata matokeo, bahati nzuri wenzetu wa nje wamekamilisha kazi hiyo na wakasema Tanzania imepata change katika malipo yale yaliyofanywa; je, uchunguzi wa ndani wa Tanzania utakamilika lini?
|
| Answer From Prime Minister |
| Mheshimiwa Naibu Spika, sina jibu kwa swali la Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed lakini kama hoja ni kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TAKUKURU tutafanya hivyo lakini kwa sasa kwa kweli siwezi kusema uongo |
 |
Hon Mohamed, Hamad Rashid[CUF] |
KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI:
Ahsante sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, je, kwa hii change ambayo tuliahidiwa kama ipo Serikali iko tayari kutumia Kamati ya Miundombinu ya Bunge ili kuhakikisha kwamba fedha yetu inakuja huku ndani? |
| Answer From Prime Minister |
| Mheshimiwa Naibu Spika, hata hili siwezi kulijibu, siwezi kulijibu kwa sababu sina taarifa juu ya jambo hili ndiyo maana nashindwa kumsaidia |
 |
Hon Slaa, Dr. Wilbrod Peter[CHADEMA] |
Mheshimiwa Waziri Mkuu, hivi karibuni Serikali kupitia Waziri wa Elimu, Mheshimiwa Profesa Jumanne Maghembe, ilitangaza kufuta ada zote za mitihani kwa wanafunzi wa shule za Sekondari, wa kidato cha pili, cha nne na cha sita. Lakini hivi karibuni vilevile kumetolewa taarifa na imenukuliwa na magazeti ya tarehe 2 Februari, 2010 akinukuliwa Afisa Habari wa Wizara kwamba, ada ziko palepale.
Vilevile hivi karibuni tumepata taarifa kutoka Wilaya mbalimbali kwamba wanafunzi bado wanatakiwa kulipa hizo ada au wazazi au walezi wao. Nini kauli ya Serikali kuhusu utata huu na, je, Serikali inasemaje kuhusu hali hii ya utata ndani ya Wizara?
|
| Answer From Prime Minister |
Mheshimiwa Naibu Spika, sidhani kama kuna utata hasa ndani ya Wizara, sidhani! Alichosema Mheshimiwa Waziri wa Elimu wakati akizungumzia jambo hili kama nilimsikiliza vizuri ilikuwa ni kwamba, utaratibu huu unaanza katika Bajeti ya mwaka unaokuja yaani 2010/2011.
Kwa sasa kwa sababu tayari baadhi ya wanafunzi walikwishalipa ada hizo tayari kwa hiyo, kutoa uamuzi kwamba ada zimefutwa bila kujali kwamba wanafunzi wengine wote wengi wameshalipa nayo haiwezi kuwatendea haki, lakini linaweza likatazamwa kwa maana ya case by case kuona kama tufanyaje kwa wale ambao genuinely wazazi wao hawana uwezo wa kulipa hiyo ada.
|
|
Records 1 to 3 of 16 |
|
|
|
|
|