|
|
| Home »Principal questions |
|
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Honourable Mtutura Abdallah Mtutura [CCM]
Tunduru Constituency |
|
| 17 |
102 |
INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT |
Communication/Infrastructure |
6 November 2009 |
Kwa kuwa Serikali kupitia wakala wa Viwanja vya Ndege nchini (TAA) wameridhika kuwa kiwanja kilichopo Mjini Tunduru kinastahili kufungwa na kuhamishiwa kijiji cha Sisi kwa Sisi na kwa kuwa suala hilo lilishapitishwa kwenye vikao vya Baraza Kuu la Halmashauri ya Wilaya na Baraza la Ushauri la Mkoa (RCC):-
(a) Je, ni lini TAA watatoa waraka wa kukabidhi eneo la kiwanja kwa Halmashauri ya Wilaya ili lipangiwe matumizi mengine?
(b) Je, Serikali haioni kuwa ucheleweshaji huo wa muda mrefu unaendeleza kero kwa wananchi na Halmashauri husika?
|
| ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #102 SESSION # 17 |
 |
Answer From Hon. Kawambwa, Dr. Shukuru Jumanne
INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT |
|
WAZIRI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mtutura Abdallah Mtutura, Mbunge wa Tunduru, lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muda mrefu kiwanja cha Ndege cha Tunduru kimekuwa katika mazingira yanayohatarisha usalama wa usafiri katika maeneo yanayozunguka kiwanja. Aidha, kiwanja hiki kimekuwa na njia za waendao kwa miguu, baiskeli na pikipiki ndani yake na wakati mwingine kuwepo kwa mifugo na hivyo kuhatarisha usalama wa ndege na abiria wakati wa kutua na wakati wa kuruka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na hali hii uongozi wa Wilaya baada ya kushauriana na watalaam wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege walikubaliana kukifunga kiwanja cha Tunduru kuanzia mwezi Machi, 2009 na kuamuliwa huduma za usafiri wa anga zihamishiwe kwa muda katika Kiwanja cha Ndege cha Matemanga ambacho kinamilikiwa na taasisi ya dini. Kwa lengo la muda mrefu, uongozi wa Wilaya ya Tunduru ulikubali kutoa eneo kubwa katika kijiji cha Sisi kwa Sisi umbali wa kilometa 16 kutoka Tunduru Mjini ili litumike kujenga kiwanja kipya cha ndege. Kazi ya kuainisha eneo hilo ilikwishafanyika na mipaka yake kutambulika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ili Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) iweze kukabidhi rasmi eneo ambalo sasa limefungwa kwa Halmashauri ya Wilaya taratibu za kisheria za kufuta kiwanja hiki kutoka kwenye orodha ya viwanja vya ndege vya Serikali lazima zikamilike kwanza. Kwa sasa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege iko kwenye mchakato wa kukamilisha taratibu zinazotakiwa za kufuta kiwanja hiki. Taratibu hizo ni pamoja na kukamilisha makubaliano ambapo shughuli za usafiri wa anga zitahamishiwa kwa muda na kuwasiliana na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) ili kiwanja cha ndege cha Tunduru kiweze kufutwa rasmi katika orodha ya Viwanja vya Serikali. Matarajio yetu ni kwamba ifikapo Desemba, 2009 zoezi hili litakuwa limekamilika na Wilaya ya Tunduru itakabidhiwa rasmi eneo hilo.
|
|
Records 1 to 1 of 10 |
|
|
|
|
|