|
|
| Home »Principal questions |
|
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Honourable Kabwe Zuberi Zitto [CHADEMA]
Kigoma Kaskazini Constituency |
|
| 16 |
102 |
EAST AFRICAN CO-OPERATION |
East Africa Co-operation |
24 June 2009 |
Kwa kuwa, katika Mkutano wa Kumi na Mbili wa Bunge na wa Bunge la Tisa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, niliomba Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wa mwaka 2010 (ambapo Tanzania itachukua Uenyekiti) ufanyike Kigoma na Serikali ikasema inatafakari ombi hilo.
(a)Kwa kuwa, kuna faida kubwa kwa miji inayoandaa Mikutano kama hiyo kama vile kutangazwa na kuongeza watalii na wawekezaji; na kwa kuwa, sasa kuna facilities za kutosha kuandaa Mkutano huo kwa kuwa hifadhi za Gombe na Mahale zinaweza kutoa fursa kwa Marais kuona utajiri wa maliasili tulizonazo.
Je, Serikali iko tayari kuanza mchakato wa mkoa wa Kigoma kuwa mwenyeji wa Mkutano huo?
(b) Je, Serikali ipo tayari kulifanya jambo hili liwe desturi ili miji mingi nchini ifaidike na EAC?
|
| ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #102 SESSION # 16 |
 |
Answer From Hon. Mohamed, Mohamed Aboud
EAST AFRICAN CO-OPERATION |
|
NAIBU WAZIRI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda nikupongeze kwa vazi rasmi la viwango. Kwa ruhusa yako na kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kabwe Zuberi Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya kwa kuomba mkutano huo ufanyike nje ya Makao Makuu ya Jumuiya kunaambatana na gharama mbalimbali.
Kwa mujibu wa taratibu za Jumuiya ya Afrika Mashariki nchi ikiomba kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi, inatakiwa kulipia gharama za Mkutano kama vile Ukumbi, Shajala, Uchapishaji, Maji, chai, chakula, burudani, gharama za usafiri kwa wajumbe wakati wa mkutano na kadhalika.
Aidha, Nchi iliyoomba hulazimika kulipia gharama za usafiri, malazi na posho ya kujikimu kwa Watumishi wa Makao Makuu ya Jumuiya watakaoshiriki kwenye Mkutano huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na maelezo niliyotoa hapo juu, hivyo kuomba kuwa mwenyeji wa mikutano ya aina hiyo nje ya Makao Makuu ya Jumuiya ni ya gharama kubwa. Kwa hiyo, itategemea sana na hali ya kiuchumi. Hali ya kiuchumi ikiruhusu kufanyika kwa mikutano ya aina hiyo kwa Kigoma na kwingineko linaweza kuwa jambo zuri kwa maendeleo ya kiutalii na uwekezaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha naomba nichukue fursa hii kuupongeza uongozi wa Mkoa wa Kigoma, akiwemo na Mheshimiwa Mbunge, kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuutangaza Mkoa wa Kigoma, kiutalii na uwekezaji.
|
|
Records 1 to 1 of 25 |
|
|
|
|
|