|
|

Hon.Samuel Sitta(MP)
Online interactive forum with the SPEAKER |
|
" One of the core duties of the Legislature is to oversee the functions of the Government in power and advise it appropriately whenever any pertinent issue of national interest arises. " |
| 5th March 2009 - Dar es Salaam. |
|
|
 |
Tender for the Financial year 2010/2011
Read more |
|
Parliamentary Resources
National Website
Prime Minister's Office website
National Electoral Commission website
Africa4All project
|
|

|
|
|
|
| Table or Tabling |
When MPs hand in questions, amendments to Bills or notices of motions or when a document is formally placed before the House. |
| Who is the Prime Minister? |
When the results of a General Election are known the President appoints the Prime Minister who becomes the leader of the Government in the Parliament. The Leader of Government Business in the House is the Prime Minister who is assisted by all Ministers concerned primarily for organising the Business and for providing reasonable facilities for the House to debates matters about which it is concerned. The current Prime Minister is the Hon. Mizengo Kayanza Pinda MP. |
Read more
|
|
|
|
|
| Home »Principal questions |
|
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Honourable Peter Joseph Serukamba [CCM]
Kigoma Mjini Constituency |
|
| 4 |
121 |
PUBLIC SECURITY AND SAFETY |
Security |
30 June 2006 |
Kwa kuwa, uvuvi ni njia mojawapo ya kuondoa umasikini kwa watu wa Kigoma; na kwa kuwa, uvuvi ndani ya Ziwa Tanganyika umekuwa sio salama, kwani wavuvi wengi wanavamiwa wakiwa Ziwani na kunyang¿anywa mali zao na kuhatarisha uhai wao:-
(a) Je, ni lini Serikali itafanya mpango madhubuti wa kulinda raia wake wakiwa Ziwani?
(b) Je, kuna utaratibu wowote wa kuwafidia watu wanaonyang¿anywa mali zao na kuhatarisha uhai wao?
|
| ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #121 SESSION # 4 |
 |
Answer From Hon. Mohamed, Mohamed Aboud
PUBLIC SECURITY AND SAFETY |
|
NAIBU WAZIRI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Usalama na Raia, napenda kumjibu Mheshimiwa Peter Serukamba, Mbunge wa Kigoma Mjini, swali lake lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-
(a) Mheshimiwa Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Serukamba kwamba yamekuwepo matukio ya wavuvi kunyang¿anywa mali zao. Serikali inalitambua tatizo hilo na inachukua jitihada ili kuimarisha ulinzi kwa kuongeza nguvu katika Vituo vidogo vya Polisi vya Kibirizi, Kagunga, Sigunga, Mgambo na Kalya.
Mheshimiwa Spika, pamoja na kuongeza nguvu za Jeshi la Polisi hivi sasa linaendelea kukamilisha matengenezo ya boti za doria, ambapo mara baada ya matengenezo kukamilika itasaidia kuimarisha ulinzi katika eneo hilo. Aidha, Jeshi la Polisi lina mpango wa kununua boti mpya za doria kwa ajili ya ulinzi katika Maziwa Makuu na Baharini.
Mheshimiwa Spika, Serikali pia inaendelea na mazungumzo ya pamoja na nchi jirani ili kuona namna ambavyo wahamiaji na wageni haramu watakavyoweza kudhibitiwa na kurejeshwa makwao.
(b) Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali haina sheria ya kuwalipa fidia wananchi waliojiajiri wenyewe. Hata hivyo, wavuvi hao wanayo fursa ya kujiwekea Bima za maisha na mali zao.
|
|
Records 1 to 1 of 12 |
|
|
|
|
|