|
|
| Home »Principal questions |
|
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Honourable Grace Sindato Kiwelu [CHADEMA]
Special Seat |
|
| 2 |
100 |
AGRICULTURE, FOOD SECURITY AND CO-OPERATIVES |
Food/Agriculture |
17 February 2006 |
Kwa kuwa Serikali itaanzisha mradi wa upatikanaji wa pembejeo kwa wakulima:-
(a) Je, Serikali inaweza kueleza idadi ya Wilaya na viwango vya fedha zilizotolewa kusaidia upatikanaji wa pembejeo hizo?
(b) Je, mikopo hiyo ya pembejeo za kilimo inasimamiwa na nani na kwa ngazi ipi?
|
| ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #100 SESSION # 2 |
 |
Answer From Hon. Chiza, Christopher Kajoro
AGRICULTURE, FOOD SECURITY AND CO-OPERATIVES |
|
NAIBU WAZIRI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Grace Sindato Kiwelu, Mbunge wa Viti Maalum, napenda kutoa maelezo ya utangulizi kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali tayari inao Mradi wa Upatikanaji wa Pembejeo kwa kupitia Mfuko wa Pembajeo (The National Agricultural Input Trust Fund) ulioanzishwa mwaka 1994 kwa Sheria ya Bunge Na. 9 ya mwaka 1994. Lengo la mfuko ni kutekeleza sera ya Serikali ya kuhakikisha kwamba wakulima wanapata pembejeo za kilimo kwa wakati na kwa bei nafuu kwa kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa waagizaji wa pembajeo ili kuwawezesha kugharamia uagizaji na usambazaji wa pembajeo za kilimo, mifugo na zana za kilimo.
Baada ya kutoa maelezo haya ya utangulizi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Grace Sindato Kiwelu, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-
(a) Mheshimiwa Spika, kuanzia msimu wa mwaka 1995/1996 hadi Juni 30,1999, Mfuko wa Pembejeo umetoa mikopo 259 yenye thamani ya shilingi bilioni 5.8 kwa wasambazaji wa pembajeo za kilimo na mifugo kwenye Wilaya 50. Hata hivyo, kuanzia msimu wa mwaka 1999/2000 hadi 2001/2002, mfuko ulisitisha utoaji wa mikopo kutokana na mikopo kutorejeshwa kwa wakati katika kipindi hicho.
Baada ya kuboresha taratibu za ukopaji na Serikali kuanza kutoa fedha, kati ya mwaka 2002 na 2005, Mfuko wa Pembejeo umetoa mikopo 730 yenye thamani ya shilingi bilioni 14.1 kwenye Wilaya 69 kwa wasambazaji wa pembejeo za kilimo na mifugo, Vyama vya Msingi vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS).
(b) Mheshimiwa Spika, mikopo ya pembajeo za kilimo husimamiwa na uongozi wa mfuko wa chini ya Bodi ya Wadhamini wa Mfuko katika ngazi ya Taifa. Aidha, katika ngazi ya Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya na Afisa Kilimo wa Wilaya wanahusika katika kusimamia mikopo hiyo kwa kuthibitisha kuwa mwombaji anastahili kupewa mkopo husika kabla ya kupitisha maombi yake na kuyawasilisha kwenye mfuko wa pembejeo.
Mheshimiwa Spika, maombi yote yaliyopokelewa yanafanyiwa tathmini na yaliyotimiza masharti yana wasilishwa kwenye Bodi ya Wadhamini. Waombaji walioidhinishwa na Bodi hujulishwa ili kuweza kukamilisha taratibu za kupata mikopo husika. Mfuko wa Pembejeo kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya hufuatilia matumizi ya mikopo pamoja na marejesho yake.
|
|
Records 1 to 1 of 11 |
|
|
|
|
|