|
|
| Home »Principal questions |
|
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Honourable Richard Mganga Ndassa [CCM]
Sumve Constituency |
|
| 14 |
105 |
EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING |
Secondary Education |
5 February 2009 |
Kwa kuwa, baadhi ya shule za sekondari za Serikali hapa nchini hupatiwa magari au pikipiki kama vitendea kazi.
(a)Je, ni sifa gani zinazofanya baadhi ya shule kupata vitendea kazi na zingine zisipate?
(b)Je, shule za Sekondari za Sumve Girls na Talo Sekondari hazistahili kupata vitendea kazi hivyo na kama zinastahili zitapata lini?
|
| ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #105 SESSION # 14 |
 |
Answer From Hon. Mahiza, Mwantumu Bakari
EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING |
|
NAIBU WAZIRI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Richard Ndassa, Mbunge wa Sumve, lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, nia ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kila sekondari inakuwa na gari ili liweze kutoa huduma mbalimbali. Hata hivyo kutokana na ufinyu wa Bajeti si rahisi kwa kila shule ya sekonari kupatiwa gari.
Wizara imeifanyia kazi suala la shule ya sekonari ya Sumve na tutaliingiza katika Bajeti ya mwaka 2009/2010. Hivyo tunamwomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira.
|
|
Records 1 to 1 of 18 |
|
|
|
|
|