ASK THE SPEAKER
GIF

Hon.Samuel Sitta(MP)
Online interactive forum with the SPEAKER
QUOTES FROM THE SPEAKER
" One of the core duties of the Legislature is to oversee the functions of the Government in power and advise it appropriately whenever any pertinent issue of national interest arises. "
5th March 2009 - Dar es Salaam.
INVITATION FOR TENDERS
Tender for the Financial year 2010/2011
Read more
RESOURCES LINKS

Parliamentary Resources
National Website
Prime Minister's Office website
National Electoral Commission website
Africa4All project

WEBMAIL LOGIN


NEWSLETTER
Subscribe to our e-newsletter and be the first to know about new activities, events and resources.
Your email
GLOSSARY
Parliament
is the highest legislative authority in the United Republic of Tanzania – the institution responsible for making and repealing Tanzania law. The Parliament is a place for reasoned discussion.
Government
is the institution that runs the country. It is also known as the Executive. The Government formulates policy and introduces legislation in Parliament.
Read more
VISITORS TO THIS SITE
There have been 30572892 visitors to this websiteThere have been 30572892 visitors to this websiteThere have been 30572892 visitors to this websiteThere have been 30572892 visitors to this websiteThere have been 30572892 visitors to this websiteThere have been 30572892 visitors to this websiteThere have been 30572892 visitors to this websiteThere have been 30572892 visitors to this website
User online : 13
Home »Answers
Principal question
  email E-mail this to a friend email Printable version
Honourable Faida Mohamed Bakar  [CCM]
Special Seat
Session No Principal Question No To the Ministry of Sector Date Asked
2 21 COMMUNITY DEVELOPMENT, GENDER AND CHILDREN Women/Women Fund 8 February 2006
Kwa kuwa akina mama wengi wa Kisiwa cha Pemba ni wafanyabiashara wazuri na hufanya biashara zao kwa kutegemea mikopo; na kwa kuwa kuna mikopo inayotolewa na benki tofauti na ile ya PRIDE Tanzania lakini ina masharti magumu na riba kubwa jambo ambalo linawarudisha nyuma akina mama hao kimaendeleo.

(a) Je, Serikali inawasaidiaje kina mama hao ili kujikwamua na hali ngumu ya maisha?

(b) Je, isingekuwa vema suala la ukubwa wa riba nalo likaangaliwa?

ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #21 SESSION # 2
Answer From Hon. Burian, Dr. Batilda Salha
COMMUNITY DEVELOPMENT, GENDER AND CHILDREN
NAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Faida Mohamed Bakar, kwa kuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya wanawake. Pia ninawapongeza akina mama wa Kisiwa cha Pemba kwa kuwa wafanyabiashara na wajasiriamali wazuri. Hii inaonyesha ni jinsi gani wanathubutu kuomba mikopo na kujiingiza katika biashara, kujiletea maendeleo yao.

Mheshimiwa Spika, nakubaliana kabisa na Mheshimiwa Faida Mohamed Bakar, kuwa mikopo inayotolewa na Mabenki na Taasisi mbalimbali za fedha zina masharti magumu. Mfano kuhitajika kuwa na dhamana ya mali zisizohamishika kama hati ya nyumba, gari na ardhi, kuwa na biashara zilizo rasmi na akaunti ambayo huwafanya wanawake wa kipato cha chini washindwe kupata mikopo.

Mheshimiwa Spika, aidha, baadhi ya Benki na Taasisi zisizo za Kiserikali hutoza riba kubwa kwa viwango tofauti kulingana na gharama za uendeshaji kwa mfano Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) 21%, Benki ya Maendeleo Vijijini (CRDB) 21%, Benki ya Posta 19.2%, National Micro Finance Bank (NMB) 24% na Taasisi kama Credit Scheme for Productive of Women in Tanzania (CREW-T) 22%.

Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa maelezo hayo ya utangulizi napenda kumjibu Mheshimiwa Faida Mohamed Bakar, swali lake lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, Serikali ilianzisha Mfuko wa Maendeleo wa Wanawake Tanzania Bara na Mfuko wa Kujitegemea Zanzibar ambayo ina masharti nafuu. Mfuko wa Kujitegea uliopo Zanzibar ambao pia una ofisi zake Pemba umeweza kukopesha mwanamke mmoja, mmoja na katika vikundi. Mfano kikundi cha Jambonia Cooperative Society kilichopo Wawi kimepata mkopo na kinajishughulisha na shughuli za ushonaji ili kujikwamua na hali ngumu ya maisha. Mifuko hii ni mifuko pekee ambayo inawafikia wanawake katika ngazi zote za chini, nchi nzima waweze kufaidika.

Mheshimiwa Spika, Serikali pia imeendelea kuhimiza na kusaidia wanawake wengi kuunda Vyama vya Ushirika vya Kuweka na Kukopa (SACCOS) na (SACAS) ambavyo vinatoa riba nafuu na kumwezesha mwanamke kujenga tabia ya kujiwekea akiba. Mfano Rombo, Kilimanjaro riba ni asilimia 10 - 13 kutegemea na makubaliano ya wanachama wenyewe.

Mheshimiwa Spika, Serikali inafanya jitihada za kuhamasisha na kuwaelimisha Maafisa Maendeleo ya Jamii juu ya mbinu za kuwahamasisha wanawake ili kuweza kujiunga na SACCOS na SACAS na kuanzisha vikundi vya kuwawezesha kukopa kwa kujidhamini wenyewe.

Aidha, jitihada zingine zinazochukuliwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine katika kuhakikisha kwamba akina mama wanaondokana na hali ngumu za kiuchumi, ni pamoja na kuwapatia mafunzo ya ujasirimali ili kuwawezesha akina mama hao kubuni biashara, kupanga na kuendesha biashara zao kwa ufanisi zaidi.

Mheshimiwa Spika, mafunzo hayo ni muhimu, kwani yanawaongezea uwezo ambao wengi wao umewawezesha kupata mikopo kwenye Benki na Taasisi mbalimbali za fedha.

Mheshimiwa Spika, ili kuwaondolea wanawake baadhi ya vikwazo vya kupata mikopo katika taasisi mbalimbali za fedha, Serikali imeweka Sheria ya Ardhi ambayo inawawezesha wanawake kumiliki raslimali ya ardhi. Sheria hiyo kama ilivyorekebishwa mwaka 2004 inawezesha ardhi kutumika kama dhamana ya kupata mikopo. Vile vile Serikali imeanzisha mpango wa kurasimisha mali (MKURABITA), mpango ambao utawezesha wanawake kutumia biashara ndogo ndogo wanazofanya kama dhamana ya kukopa.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea na mchakato wa uanzishwaji wa Benki ya Wanawake. Tunatarajia kuwa Benki hii itakapoanzishwa wanawake wanachama wa Vyama vya Ushirika na vya kuweka na kukopa wataweza kufaidika na mikopo kupitia Benki hii.

(b) Mheshimiwa Spika, hata hivyo nakubaliana kabisa na Mheshimiwa Mbunge kuwa ukubwa wa riba ni jambo ambalo linahitaji kuangaliwa kwa makini. Sera ya National Micro Finance ya mwaka 2000 imeelekeza kuwa Taasisi za kifedha ndizo zitakazojipangia riba za mikopo wanayotoa.

Aidha, suala la riba kibiashara ni suala ambalo hutawaliwa na vigezo mbalimbali vikiwemo vya mfumuko wa bei, gharama za usimamizi na uendeshaji na kutokana na hali hiyo suala la ukubwa wa riba ni changamoto. Kulingana na vigezo hivyo inakuwa vigumu kwa Serikali kudhibiti viwango vya riba hasa katika mabenki ya biashara.

Mheshimiwa Spika, napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa Serikali inaangalia suala hili la riba kama changamoto kwetu. Hivyo basi kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 Ibara ya 120, ninanukuu, ¿Tutaendelea kujenga mazingira mazuri ya kuziwezesha benki na asasi nyingine zinazotoa huduma ya mikopo kutoa mikopo kwa masharti nafuu kwa wanawake miongoni mwa wananchi wote,¿ mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, napenda kutoa changamoto kwa wanawake wajiunge na kuanzisha vikundi au vyama vyao vya kuweka na kukopa ili waweze kusimamia na kupanga riba iliyo nafuu kulingana na mazingira yao.

Aidha, Serikali itaendelea kutoa mafunzo ya ujasirimali ili wanawake wengi zaidi wajue umuhimu wa kukopa, umuhimu wa kurejesha mikopo na umuhimu kuanzisha biashara ambazo zitawapatia faida na hatimaye kujiwekea akiba kwa maendeleo yao.
Records 1 to 1 of 44
 
Next Last
WHO IS WHO
Hon.Al-Qassmy, Khadija Salum Ally
bunge
Questions(2)
Supplementary Questions(3)
Contributions(64)
More Members »


POLIS DATABASE
polis
BUDGET 2010/11
Estimate of Public Expenditure Development votes and supply vote
SEARCH FOR MP
Region
Constituent
 
VIDEO /AUDIO CLIP
More Videos
PHOTO GALLERY
President Kikwete posing in a group picture when he visited Bunge - Dodoma on 21.8.2008.
More photos
CALENDAR OF EVENTS
 <<  < Sep 2010 >   >>
SMTWThFS
1234
5678
9
1011
12131415161718
19202122232425
2627282930

More events

Copyright © 2003-2008 Tanzania Parliament. All rights reserved.
Designed and published by DataVision International (T) Ltd
Terms of Use | Disclaimer