|
|

Hon.Samuel Sitta(MP)
Online interactive forum with the SPEAKER |
|
" One of the core duties of the Legislature is to oversee the functions of the Government in power and advise it appropriately whenever any pertinent issue of national interest arises. " |
| 5th March 2009 - Dar es Salaam. |
|
|
 |
Tender for the Financial year 2010/2011
Read more |
|
Parliamentary Resources
National Website
Prime Minister's Office website
National Electoral Commission website
Africa4All project
|
|

|
|
|
|
| Parliamentary Committees |
The services of the Speaker and his deputies, and those of the permanent officers who are at the Speaker's disposal are not the only auxiliaries to which the House has recourse for the dispatch of its work: with a view to the efficient performance of its role it is accustomed to Parliament to appoint temporary composite bodies from among its own membership, which we refer to as Committees. |
| By-elections |
A by-election occurs when a seat in the National Assembly becomes vacant during the lifetime of a Parliament (i.e. between general elections). |
Read more
|
|
|
|
|
| Home »Contribution |
|
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Omar, Juma Said[CUF]
Mtambwe Constituency |
|
|
|
|
|
| 20 |
28 |
12 July 2010 |
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2010/2011 - Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi |
Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uzima na afya na kushiriki katika kikao cha leo cha Bunge.
Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu ni ufunguo wa maisha. Elimu ndiyo inayomwezesha mwanadamu kupambana na mazingira yake kiuchumi, kisiasa na kijamii. Serikali inahakikisha vipi kwamba elimu inayotolewa nchini inamwezesha Mtanzania katika kukabiliana na sekta za kiuchimi, kisiasa na kijamii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuwepo kwa madarasa ya kutosha katika mashule mengi hapa nchini, ni hatua moja muhimu lakini kuwapo kwa Walimu wa kutosha ni hatua nyingine muhimu zaidi. Serikali inatoa tamko gani kuhusu kujitosheleza kwa Walimu wenye sifa zinazotakiwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanafunzi wanajifunza na kufahamu zaidi pale wanaposhirki katika masomo kwa vitendo hususan masomo ya sayansi. Serikali imejiandaa vipi ili kuhakikisha mashule yote ya sekondari yanapata maabara yenye vifaa kamili vinavyohitajika kwa masomo hayo ya sayansi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mipango gani itakayohakikisha kwamba wanafunzi wanapata vifaa vya kusomea na kujifunza kuanzia ngazi ya Msingi, Sekondari hadi Vyuo Vikuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ili Mwalimu aweze kufanya kazi yake vizuri na kwa ufanisi, anahitaji maslahi bora pamoja na makazi bora. Serikali inasema nini kuhusu uboreshaji wa maslahi pamoja na maakazi ya Walimu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanafunzi walemavu wanasoma katika mazingira magumu. Serikali ina mpango gani wa kuboresha mazingira ili wanafunzi walemavu walio wengi waweze kufikia Sekondari na Vyuo Vikuu badala ya kuishia Elimu ya Msingi tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, posho ya chakula na malazi kwa wanafunzi wa elimu ya juu, ni ndogo mno kiasi kwamba hailingani na gharama za maisha. Baadhi ya wanafunzi wanalazimika kulala nje ya vyuo vyao kutokana na uchache wa vyumba vya kulala jambo ambalo linaleta usumbufu kwa wanafunzi hao, Serikali inaiboreshaje hali hii?
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mpango gani maalum wa kukomesha tatizo la vyeti vingi vya kughushi pamoja na udanganyifu katika mitihani kuanzia Msingi hadi Vyuo Vikuu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mpango gani wa kuzipatia umeme shule za sekondari?
|
|
Records 1 to 1 of 53 |
|
|
|
|
|