|
|
| Home »Contribution |
|
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Seif, Ali Khamis[CUF]
Mkoani Constituency |
|
|
|
|
|
| 20 |
19 |
29 June 2010 |
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2010/2011 – Wizara ya Miundombinu |
Mheshimiwa Spika, katika suala la ujenzi katika maeneo mbalimbali udhibiti wake unafanywa na aidha na Manispaa au Mamlaka ya Majengo Tanzania (TBA). Kuna mgongano mkubwa baina ya TBA na Manispaa katika suala zima la ruhusu ya ujenzi katika Manispaa. Tatizo hilo limetokea katika Halmashauri ya Manispaa ya Tanga na Kinondoni. Nataka nieleweshwe ni nani hasa mwenye Mamlaka ya ruhusa ya ujenzi katika maeneo hayo?
Nchi yetu imepakana na nchi kadha ambazo hazina bandari. Sisi tumebahatika sana kuwa na Bandari ya Mtwara, Lindi, Dar es Salaam, Tanga na Zanzibar. Wingi wote huo wa bandari bado tumeshindwa kuzihudumia ipasavyo nchi zilizotuzunguka. Bado utendaji wa Bandari zetu ni mdogo na zina urasimu mkubwa, inachukuwa siku nyingi wateja kupata mizigo yao. Usafirishaji wa mizigo kwa kukosa reli yenye uhakika ni tatizo na kwa kupitia kwenye barabara kuna usumbufu mkubwa ukiwemo vituo vingi vya gari hizo kusimama kwa visingizio mbalimbali. Bila ya kuziboresha Bandari zetu, reli na huduma kwenye barabara zetu, nchi zinazotuzungunguka zitaelekea nchi nyingine kupata huduma hizo.
Mheshimiwa Spika, ni aibu sana nchi yetu kuwa na Shirika la Ndege (ATCL) lisilo na uhakika na usafiri zake za nje ya nchi lakini hata kwa safari za ndani. Kila bajeti Wizara inaeleza kuwa wataliimarisha shirika hilo lakini inavyoonekana ni maneno tu. Nchi yetu ina vivutio vingi vya utalii lakini biashara ya utalii haiwezi kuimarika bila ya kuwa na Shirika letu la Ndege. Ni lini Shirika hili litaweza kukidhi haja inayokusudiwa badala ya maneno ya kawaida yanayosemwa hapa Bungeni.
Mheshimiwa Spika, watu wengi wanapoteza maisha yao aidha kwa kusafiri kwenye Bahari yetu au kwa uvuvi lakini hakuna chombo maalumu cha uokoaji wa maisha ya wananchi hao. Nadhani umefika wakati kuanzishwa kikosi maalum cha uokoaji badala ya kutegemea Kikosi cha Polisi cha Bahari, Kikosi cha Bandari ni watu binafsi. Ninashauri kiundwe Kikosi cha Ulinzi wa Ukanda wa Bahari (Coast Guard) kazi yake iwe ni ulinzi wa Ukanda wa Bahari yetu na uokozi wa wananchi wetu.
Mheshimiwa Spika, ukiangalia ukurasa 74 wa Hotuba ya Waziri, kifungu cha 94, abiria waliosafirishwa kwa meli katika Maziwa Makuu kwa mwaka 2009/2010 ni 474,252 na kifungu 95 kwa mwaka 2010/2011 ni abiria 475,715 wataosafirishwa na meli katika Maziwa Makuu. Ni dhahiri tofauti iliyopo ya abiria watakaosafirishwa kwa mwaka 2009/2010 na 2010/2011 ni 1,464, hili ni ongezeko dogo. Ongezeko hilo dogo limetokana na changamoto zinazolikabili Shirika la MSCL. Ipo haja changamoto hizo zitafutiwe ufumbuzi.
Mheshimiwa Spika, ahsante.
|
|
Records 1 to 1 of 55 |
|
|
|
|
|