|
|
| Home »Contribution |
|
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Serukamba, Peter Joseph[CCM]
Kigoma Mjini Constituency |
|
|
|
|
|
| 20 |
19 |
29 June 2010 |
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2010/2011 – Wizara ya Miundombinu |
| Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilitaka kupata maelezo kuhusu Shirika la Ndege la ATCL. Pamoja na maelezo mazuri ya Waziri kwamba tumeongea na mfadhili lakini mimi nilidhani tungekuja na mkakati, nilitaka sasa Waziri aniambie kuna mkakati gani kwanza kama nchi tusafishe madeni ambayo tunadaiwa, tulipe baada ya kufanya biashara miaka miwili, mitatu tunaanza kupata faida ndiyo tuanze kwenda kuongea na mtu wa kuja kuingia naye mkataba kama partner, sasa ukienda wakati vitabu ni vichafu hata namna ya ku-negotiate huwezi ku-negotiate kwa sababu unakwenda wewe almost kampuni imekufa, matokeo yake utafanya anachotaka yeye yule unayemuita kuja kuingia naye ubia. Mimi nilitaka Waziri aniambie kwenye kitabu cha maendeleo hapa sioni pesa yoyote kwa ajili ya ATCL na kweli watu wengine kama sisi ndege hiyo kwa watu wa Tabora na Kigoma ni ya muhimu sana, moja ninachotaka kujua mkakati wa Kibajeti wa kwetu kwanza kabla ya huyu Mchina au mwingine ukoje kwenye suala hili? |
|
Records 1 to 1 of 60 |
|
|
|
|
|