9 September 2010
ASK THE SPEAKER
GIF

Hon.Samuel Sitta(MP)
Online interactive forum with the SPEAKER
QUOTES FROM THE SPEAKER
" One of the core duties of the Legislature is to oversee the functions of the Government in power and advise it appropriately whenever any pertinent issue of national interest arises. "
5th March 2009 - Dar es Salaam.
INVITATION FOR TENDERS
Tender for the Financial year 2010/2011
Read more
RESOURCES LINKS

Parliamentary Resources
National Website
Prime Minister's Office website
National Electoral Commission website
Africa4All project

WEBMAIL LOGIN


NEWSLETTER
Subscribe to our e-newsletter and be the first to know about new activities, events and resources.
Your email
GLOSSARY
Amendments
When Members of the Parliament are debating or examining Bills they often want to change some of the details. They can therefore propose changes or amendments, and debate and vote on them in the House. konya haber konhaber
Code of Conduct
helps MPs understand their responsibilities to Parliament and the public. In addition to guidance, the Code also requires all Members to declare outside interest, like paid work or gifts
Read more
VISITORS TO THIS SITE
There have been 30573000 visitors to this websiteThere have been 30573000 visitors to this websiteThere have been 30573000 visitors to this websiteThere have been 30573000 visitors to this websiteThere have been 30573000 visitors to this websiteThere have been 30573000 visitors to this websiteThere have been 30573000 visitors to this websiteThere have been 30573000 visitors to this website
User online : 13
Home »Contribution
Contribution
  email E-mail this to a friend email Printable version
Nyalandu, Lazaro Samuel[CCM]

Singida North Constituency
Session No Seating No Contribution Date Contribution To
19 8 22 April 2010 Muswada wa Sheria ya Madini wa Mwaka 2010 (The Mining Bill, 2010)
Mheshimiwa Spika, nachukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunipa nafasi hii, naomba kusema tuna imani na uongozi wako. Pia nichukue nafasi hii ya kipekee kumshukuru sana Mheshimiwa William Ngeleja, kumpongeza akishirikiana na Mheshimiwa Adam Malima kwa uhodari wao kwa kazi nzuri waliyoifanya kutafsiri kwa haraka maagizo na utashi wa Mheshimiwa Rais kwamba Sheria ya Madini ije kwa agency kwa certificate of agency, ifanye haraka kabla ya uchaguzi wetu mkuu.

Mheshimiwa Spika, naomba nichukue nafasi kuwapongeza na niliwaambia nje, ndugu David Jailo pamoja na Dr. Peter Kafumu, kazi waliyoifanya katika maandalizi ya sheria hii inakuwa mfano wa kuigwa kwa watendaji wengine wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hii kuipongeza kwa dhati Kamati ya Mheshimiwa Shellukindo, kazi mliyofanya kwa niaba yetu ni nzuri inatukuka na inaheshimika, alitajwa na naomba nimtaje kipekee Mheshimiwa Andrew Chenge, mchango wake wa dhati umekuwa mzuri na naomba nitaje hapa kwamba tunakushukuru kwa niaba ya Watanzania wote ambao sasa wataipata sheria hii.

Mheshimiwa Spika, naongea kwa niaba ya mikoa yote yenye madini, mikoa yote isiyo na madini wachimbaji wanaonisikiliza wa pale Mpambaa, Singida, walioko katika Tarafa ya Mtinko, wale wa Ilongero Mgori maeneo ya Londoni pale Manyoni na sehemu zote katika nchi hii. Sheria hii ambayo Serikali inaileta ni sheria nzuri sana.

Mheshimiwa Spika, wote tunafahamu na mengi yameelezwa, Tanzania kuwa nchi ya tatu kwa deposit ya madini ya dhahabu ukiacha Afrika ya Kusini na Ghana na habari ambazo tunazipata ni kwamba Tanzania hivi karibuni itaizidi Ghana kutokana na uvumbuzi mbalimbali unaoendelea. Nchi hii ndiyo sehemu pekee yenye Tanzanite, nchi hii ina utajiri mkubwa, nchi hii ni nchi chache katika Afrika ambako watu wangependa kwenda, wakae wajisikie vizuri, hivi karibuni wale waliokuwa wakimbizi katika nchi yetu kutoka nchi ya jirani. Umoja wa Kimataifa umetupongeza kwa kuwapa uraia nchi hii inapendwa na wageni, inapendwa na wenyeji, ni nchi ya heshima na tunaendelea kumwomba Mungu awabariki na Mungu awabariki wenyeji wa nchi hii katika kuendelea kuifanya nchi yetu iwe ya heshima zaidi.

Mheshimiwa Spika, sheria hii kwa maneno mafupi na kwa kuitazama inatafsiri kwa uhakika kabisa jinsi ambavyo nchi yetu itauchukua utajiri tulionao wa ardhini uwe utajiri wa matumizi wealth of the nation nchi yetu ifike mahali kama watoto wanavyoimba tunapokwenda kwenye kampeni, wanaimba CCM bomba, mgombea huyu ni bomba sana, naomba watoto wale katika shule zetu waendele kuimba Tanzania ni nchi bomba.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu nchi hii ni nchi nzuri, ni nchi ambayo tunaitazama kwa matumaini makubwa na nashukuru sana kwa mara ya kwanza sheria ya madini inakita kwa walichosema wenzangu uhimili wa Serikali katika kushiriki sehemu ya hisa kwa ajili ya wananchi wa sasa na vizazi vijavyo.

Mheshimiwa Spika, hivi karibuni nilitembelea Botswana ni nchi ambayo inaendeshwa na wingi wa ng’ombe, wakulima wana ng’ombe wengi sana. Jambo la pili wana almasi diamond, halafu la tatu na la mwisho wana Hifadhi za Taifa. Mpango wao wa kufanya almasi ya nchi hiyo iwe inakuwa processed katika Gaboloni. Jambo la kwanza wameiongezea heshima nchi hiyo, Serikali imeshika hisa nyingi sana kwa niaba ya wananchi na watu chini ya milioni tatu ina utajiri mkubwa sana katika Afrika ukiacha Afrika ya Kusini.

Mheshimiwa Spika, heshima ya Botswana imepanda, nchi nyingine ni Sierra Leon, wenzetu hawa wana almasi, sinema ya hivi karibuni ikachezwa wanaita blood diamond, maana yake wenzetu waliamua kuzipiga kweli kweli kwa sababu ya dhahabu walizonazo. Nchi yetu ina heshima ya amani, ni matumaini yangu kwamba rasilimali hizi na kwa sheria hii kukubali kushika sehemu ya hisa kwa niaba ya wananchi italeta heshima sana. Napongeza sana nia hiyo ya Serikali na juhudi hiyo za Serikali kuweza kuiweka hii katika sheria.

Mheshimiwa Spika, ni imani yangu kwamba kwa sababu wimbo mkubwa ambao unaimbwa tangu nikiwa mdogo, nchi yetu ni nchi maskini, alisema Mzee Mzindakaya, hakuna umaskini wowote katika Tanzania katika kijiji kimoja ambacho wana mifugo 2000 karibu kwa familia zaidi ya mia moja na wao wanaamini ni maskini? Watu ambao wamekaa juu ya dhahabu, juu ya almasi, juu ya madini mbalimbali, wameendelea kuamini kwamba wao ni maskini, nafikiri sheria hii inaifikisha nchi mahali ambapo tunaamini kwamba umaskini wa Tanzania ulikuwa ni umaskini wa kutokujua ni nini tulichonacho. Naomba nchi hii chini ya uongozi madhubuti wa Rais wetu na chini ya uongozi madhubuti wa Waziri wa Wizara hii kwa sheria hii tukasimame kidete tuifaidi na tuyafaidi madini ya aina mbalimbali yaliyopo katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali itakapokuwa ina-negotiate na wageni na wawekezaji mbalimbali juu ya free carried interest, ihakikishe kwamba ile negotiation inakuwa kwenye higher end, asilimia kubwa kwa kadri itakavyowezekana kwa kadri ya matakwa ya uwekezaji na masharti yatakayokuwepo wakati huo.

Mheshimiwa Spika, naomba niseme suala zima ambalo limeongelewa na wenzangu la ongezeko la thamani, suala la processing, smelting na refining litakuwa ni suala muhimu sana katika sheria hii na naiunga sana mkono Serikali kuileta sasa hivi. Wamesema wengi kuhusu ukuaji wa ajira, ongezeko la thamani kwa madini na vitu mbalimbali vitakavyozalishwa hapa vitaifanya Tanzania ijiwekee heshima na kuwa produce of Tanzania kwa sababu hata nguo ikitengenezwa China wataandika pale pembeni made in China.


Mheshimiwa Spika, dhahabu ya Tanzania itakapoanza kuuzwa popote tunataka ijulikane kwanza hii ni dhahabu ya Tanzania, tunataka tanzanite ya Serikali ijulikane kwamba hii ni tanzanite ambayo origin yake ni Tanzania. Haiwezekani ikatokea bila kuwa na processing, bila kuwa na smelting na bila kuwa na refining. Katika refining Serikali ni lazima kwa kutumia vyombo vyake wamesema wenzangu iwe na hisa. Udanganyifu mwingi sana wa makampuni ya madini ni pale ambapo tunashindwa kujua thamani ya mali tuliyonayo.

Mheshimiwa Spika, interest hii ni lazima ilindwe kwa vizazi vya sasa hivi na vizazi vingi sana vijavyo. Napendekeza kama ilivyo katika Istanbul kule Uturuki kuwe na establishment ya Tanzania gold exchange hii inatokana tu na refining na bila kuwa na gold exchange vitu vingi sana vitapotea. Naomba sana Serikali ifikirie uwezekano wa kuweka Tanzania Gold Exchange.

Mheshimiwa Spika, katika miaka 25 ijayo inakisiwa Watanzania watakuwa wamefika milioni 75 na kuendelea. Tatizo tulilonalo kiuchumi Tanzania sasa hivi ni ukosefu wa umeme wa kutosha. Of course sisi tuna hydropower resources za kutosha na capabilities. Lakini kwa kuwa katika Mkoa wa Singida, Songea na Mikoa mingi sana potential ya Uranium ni kubwa sana, madini haya ndiyo madini pekee duniani ambayo yanaweza yakatusaidia kwenye teknolojia ya nuclear power, Tanzania ikiweza kutengeneza nuclear power station moja inatosha kutoa nguvu ya nishati ya umeme kwa zaidi ya watu 50,000, usambazaji wake unakuwa mgumu kama unakwenda kila kijiji. Lakini inategemewa miaka 25 ijayo zaidi ya nusu ya Watanzania watakuwa katika maeneo makubwa ya miji.
Mheshimiwa Spika, nchi ya Kenya wameanza ku-negotiate na UN atomic agency. Naomba Tanzania tusilale kwa uwezekano wa kupata vibali, tuanze kufikiria na kuelimisha watu kuwa tayari na nuclear atomic technology katika nchi yetu katika miaka ijayo. Hivi karibuni katika Tanzania matumizi ya umeme katika Tanzania ni KH 85, katika nchi nyingi za sub Sahara Africa nchi zote tunazopambana hapa wastani wao wa matumizi kwa mwaka ya umeme ni 432 na katika dunia wastani ni 2176.

Mheshimiwa Spika, kwa maneno mengine matumizi yetu ya nguvu ya umeme ni madogo sana kwa sababu umeme wetu ni wa gharama kubwa, unapatikana kidogo na unatumika maeneo machache. Wananchi wengi wa Tanzania katika Tanzania kwa wastani leo na hizi ni kumbukumbu za mwaka 2007, asilimia 95.8 ya Watanzania wote wanapika kwa kutumia kuni na kwa kutumia mkaa. Katika Mji wa Dar es Salaam asilimia 71 leo wanapika kwa kutumia kuni na mkaa.

Mheshimiwa Spika, hizi ni takwimu za Serikali yenyewe. Ni lazima tufanye kila tunaloweza kuhakikisha kwamba vijana wanaandaliwa kwa sababu ni suala la elimu, shule zetu, vyuo vikuu vyetu vianze kuwa na vitengo vya nuclear technology, watu waanze kufundishwa, tuanze kufanya maandalizi tutakapokuwa tayari uranium tuliyonayo iweze kufanya kazi ya kuipeleka nchi yetu katika hatua nyingine. Kuna suala la balance of power katika Afrika Mashariki, Uganda wamegundua mafuta mengi sana na wengi wameanza kutembea kifua wazi.

Mheshimiwa Spika, lakini hakuna aliye na madini mengi kama alivyosema Mzee Mzindakaya na mtu mwingine kama Tanzania na The DRC ni lazima Watanzania popote waliko dunia wafahamu nchi yao ni nchi nzuri, ni nchi iliyo na endowment, ni nchi ambayo wanapaswa huko waliko watamani na wafikirie kurudi kwao huku Tanzania. Ni lazima tuandae matumizi ya rasilimali hizi kwa ajili ya ku-balance power. Rwanda wanatumia madini mengi sana ambayo hatujui yametoka wapi. Lakini unaweza ukahisi na waka-export. Tanzanite ya Tanzania inakuwa exported through Nairobi na South Africa. Tungependa Tanzanite na madini mengine yote kama nilivyosema yaonyeshe katika certificate zake origin yake ni Tanzania. Yapate kuwa registered, kodi zote zilipwe hapa Tanzania na tuhakikishe kwamba nchi yetu inasonga mbele.

Mheshimiwa Spika, pasipo kutumia maneno mengi zaidi wengi wameyasema, wachimbaji wadogo wadogo popote walipo na hasa wale wa Jimboni kwangu natumaini mnanisikia, Serikali iko pamoja na ninyi, sheria ndiyo hii Chama cha Mapinduzi, wameileta kwa ajili ya uchaguzi kuhakikisha kwamba chama hiki kinachowajali wananchi daima dumu kinaendelea kushinda.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
  Records 1 to 1 of 20
Next Last
WHO IS WHO
Hon.Kigwalilo, Hassan Chande
bunge
Liwale Constituency
Questions(26)
Supplementary Questions(31)
Contributions(32)
More Members »


POLIS DATABASE
polis
BUDGET 2010/11
Estimate of Public Expenditure Development votes and supply vote
SEARCH FOR MP
Region
Constituent
 
VIDEO /AUDIO CLIP
More Videos
PHOTO GALLERY
Police parading(Saluting)the President Jakaya Kikwete when arrived to the Bunge Complex in Dodoma on 21.8.2008.
More photos
CALENDAR OF EVENTS
 <<  < Sep 2010 >   >>
SMTWThFS
1234
5678
9
1011
12131415161718
19202122232425
2627282930

More events

Copyright © 2003-2008 Tanzania Parliament. All rights reserved.
Designed and published by DataVision International (T) Ltd
Terms of Use | Disclaimer